Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa wabunge kuzisoma na kuzitumia ipasavyo  kanuni za bunge ili kuondoa manug'uniko yanayojitokeza pindi wanapozuiliwa na spika kuchangia mijadala au kutoa hoja bungeni kwa sababu ya kukiuka kanuni na umuhimu wa waandishi wa habari  kuzitumia taarifa rasmi za bunge katika utoaji wa taarifa zao.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya kamati kuondolewa  pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3 zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.Picha na Aaron Msigwa-MAELEZO 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jana sikumuelewa kabisaa Dr. Kashilila kwamba wanapendekeza shughuli za bunge zisiwe live coverage ili waweze ku edit. Hivi kupingana kwa hoja hadharani kunawezaje kuchochea mabadiliko hasi ya vijana kitabia? Yaani wenzetu Kenya wako kwenye karne ya kufanya usahili wa nafasi zote za kazi kubwa serikalini live na hata uchunguzi wa matukio mbalimbali kama ubadhirifu wa mali kwa watuhumiwa live, sisi tunataka wabunge tuliowatuma kwa kura zetu wa edit kwanza movie zao ndio watuletee??????????????????tunaipeleka wapi nchi hiiiii??????????Kila kukicha nafuu ya jana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...