Wanafunzi wa chuo kikuu cha udaktari (Kilimanjaro Christian Medical University College) kutoka miaka mbalimbali na kozi mbalimbali wakishirikiana na wafanyakazi wa KCMC (kilimanjaro Christian Medical Centre) kupitia kikundi chao kiitwacho Shine Light wameweza kukusanya shillingi Milioni mbili na Laki saba na kuweza kuwasaidia wanafunzi 23 kutoka kituo cha kulelea watoto wanaoshi katika mazingira magumu kwa ajili ya masomo yao,wameweza kuwanunulia sare za shule (mashati,masweta,kaptura,sketi,soksi, begi, madaftari na rula) vile vile na ada ya mwaka mzima kwa wanafunzi hawa.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo.
Habari hii inapatikana kwa ufupi sana kupitia www.kitongoni.blogspot.com
Mungu awabariki sana muendelee na moyo huo huo.
ReplyDeleteMungu awabariki. Ni mfano mzuri sana kwa hao watoto na jamii kwa ujumla.
ReplyDelete