Timu inayolisuka tawi la Chadema UK imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba uongozi utakaochaguliwa una vitendea kazi vya kisasa ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Kwa hali hiyo basi tungependa kuitangaza rasmi website ya Chadema UK :
Pia kwa kuzingatia kwamba dunia ya sasa mawasiliano ya jamii ni kupitia njia mbalimbali za kiteknolojia, tunawatangazia wanaChadema UK wote kuwa sasa Chadema inapatikana facebook:
Jina: Chadema UK
Umuhimu wa mawasiliano kwa njia ya simu pia nao umepewa kipaumbele. Hata hivyo tunadhamiria kuhakisha mawasiliano hayo hayamgharimu mwanachadema. Kwa hivyo tunashughulikia kupata mobile phone yenye free text messages and calls applications (Viber, Whatsapp na Tango). Hii itarahisisha namna tunavyowasiliana na wapenda maendeleo.
Mambo yote haya yanafanyika ili kuongeza ufanisi lakini pia ni katika kuhakikisha kwamba Chadema iko karibu sana na wanachadema na watanzania wote kwa ujumla.
Hatutalala mpaka kieleweke!
People’ssss Power

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunakwenda wapi Watanzania?maoni yangu niliyo yatoa katika blog ya kwanza kuhusu uchaguzi wa viongozi wa Tawi la CCM katika nchi hiyo ya nje,maoni hayo pia yawaendee jamaa zetu wa Chadema huko UK!Hebu sote tutafakari,badala ya kukurupuka,hili linalofanyika sasa la kufungua matawi ya vyama vya siasa hususan CCM na Chadema huko Uingereza ni sahihi?na litatufikisha wapi?kwa maslahi ya nani?Kwanini tumefikia hapo?Mambo yetu ya ndani yametushinda,sasa tumeanza kukimbilia nje,je,tumefikia Ukomo wa Kufikiri?Sumu hii ya kisiasa inayolishwa vijana wetu italigawa Taifa vipande vipande!Vijana hawa wana majukumu muhimu zaidi huko nchi za nje,"za kuiba teknolojia na utaalamu wa kisayansi"ili waje walikomboe Taifa lao,lakini, siyo kuota ndoto za kuja kuwa Viongozi wa Siasa na Serikali hapa nchini,badala ya Kusoma na Kujituma!Hayo ya Uongozi watayakuta,wasiwe na papara!Lets all unite in this fro the sake of our beloved Nation!Tusigeuze Siasa kuwa "Dili"!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...