Email address:ccmwashdc@gmail.com

Ndugu Wana CCM DMV mnaombwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi bila kukosa,
 Ni nafasi ya kuwachagua viongozi wako utakao wapenda kujenga Chama imara.
SIKU: JUMAMOSI Machi 16, 2013
MUDA:  SAA 10 JIONI (4pm)
MAHALI: TUTAWATANGAZIA
 Ili uweze kupiga kura hakikisha una kadi yako ya Chama na uwe mwanachama hai, na kama huna kadi au umepoteza tafadhali wasiliana na Katibu wa Tawi wa muda
Yacob Kinyemi, Simu (202)-629-7841, email: yacob1972@yahoo.com

Nafasi zinazowaniwa ni:
1) Mwenyekiti wa tawi
2) Katibu wa Tawi
3) Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Tawi
4) Katibu wa Fedha na Uchumi wa tawi
5) Mwenyekiti wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
6) Katibu wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
7) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)
8) Katibu wa Jumuiya ya Wanawake ya Tawi (UWT)
9) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Tawi
10) Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Tawi

SIFA ZA MGOMBEA:
1.      Awe na umri kuanzia miaka 18
2.      Awe mwachama wa CCM mwenye kadi
Fomu za kugombania nafasi za uchaguzi ziwakilishwe kwa M/Kiti ( HIDAYA MAHITA)wa Kamati ya Uchaguzi kwa njia ifuatayo:
Fax: 1(888)835-5784     Email: ccmwashdc@gmail.com
Mailing address: 1709 HAMPSHIRE GREEN LANE#33 SILVER SPRING MD 20903
  
MWISHO WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU HIZO NI  TAREHE 8 MARCH 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. This is my honest sincere personal opinion:Watanzania sasa tunaelekea pabaya,I am sorry to say this!Juzi hapa niliona tangazo katika Blog hii,kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chadema somewhere in the UK,na sasa tangazo lingine la uchaguzi wa CCM,hukohuko nchi za nje!Tunapandikiza "sumu gani"kwa vijana wetu?Hawana wanacho fikiri au kubuni katika Kaa yao huko nje ili kuja kulikomboa Taifa lao kiuchumi na kiteknolojia,bali ni ndoto za Uongozi wa "siasa,siasa,siasa,siasa,siasa....inftn...."!Just what the hell is this?Mambo yetu hapa nyumbani yanatushinda,badala ya kuimarisha Mifumo ya Usimamizi wa Uchumi na Taasisi za Demokrasia ya kweli hapa ndani nchini kwetu,muda mwingi sana unapotezwa kwa vijana wetu kufikiria,kesho watakapo rudi nyumbani,watakuwa na nafasi zipi za Uongozi nchini,katika Vyama vyao vya siasa na katika Serikali!!This is a very unfortunate and unhealthy political trend?Na linapewa Upatu na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa ambao ni "Mufilisi wa Itikadi na Busara".Wakati sasa umefika kuwaasa vijana wetu wote walioko nje ya nchi,wengi wao masomoni,kwamba,wakumbuke wajibu wao kwa Taifa lao,kwa kujikita zaidi katika Masomo yaliyo wapeleka huko,wajikite zaidi katika "kuiba teknolojia za kisasa"ili waje waiendeleze nchi yao,badala ya kuingizwa Mkenge katika masuala ya Siasa,ambayo kwao sio wakati wake hivi sasa!Hii ni aibu kubwa!Eti tuna matawi ya vyama vya siasa nchi za nje,aibu gani hii?Mbona mkiwa nje hamshiriki katika Uchaguzi Mkuu kila unapofanyika hapa nchini?Hamjiulizi tu,ni kwa nini inakuwa hivyo?Kipi cha maana zaidi,kufungua matawi ya chama huko nje,au kwanza kupigania haki yenu ya kupiga kura katika kila uchaguzi mkuu kuchagua Rais wenu?Let somebody define,"what is education?"in the first place!

    ReplyDelete
  2. ANKAL EE HIVI HUU URAIA PACHA AU DUAL CITISEN ITAKUJA LINI? TUSHACHOKA ANKAL TUNATAKA TUJE TUJIAJIRI NYUMBANI SASA KWETU SIE TUKIJA VIZA MIEZI MITATU KWA STAILI HIYO KWELI KUNATUTAKACHO KIFANYA.? TUSHACHOKA ANKAL ONGEA BASI NA MNENE JAPO ASPEED UP HIYO AGENDA DAH!

    ReplyDelete
  3. Raia wa USA lazima alipe kodi USA kila mwaka hata asipoishi USA. Na sisi tuweka hii kwa wale raia wetu wanaishi nje lazima nao walipe kodi kila mwaka.

    ReplyDelete
  4. Anomymous wa kwanza! Safi Sana Mkuu " You nailed IT!!!
    Watanzania wa ughaibuni wanasahau ni kipi kilichowaleta huku nje, they tend to focus on siasa za nyumbani na kufikiria nivipi they can be part of the party ili waibe na sio kusaidia kwao... Jamani u need to Focus kwenye masomo na maisha yenu, pigeni box muzichange sio kazi kila weekend kuanda mikutano will no pay! Namnukuu mwanangu Al Pacino :- In this Country u gotta make the money First, when you get the money, you get.... malizieni wenyewe... KAZI na SHULE ndio zinatakiwa... Bwana weee nenda kwenye hizi shughuli uone wabongo English inavyowapiga chenga... Accent na pronunciation ndio mamaaaaaaaaaaaaa!!!!

    ReplyDelete
  5. wewe wa kwnza nyamaza kwani wakifungua matawi ya nakuuma nini kwani hamna watanzania huku wewe vipi ?

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Wed Feb 27, 10:50:00 am 2013

    Jamaa yangu nakubalina na wewe, lakini jamaa wengi walioko Ughaibuni wanaonzisha vyama huko ni wale wale. Hapa unapoongea na ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Wengi wao ni watoto wao wamepelekwa kusoma ili watakapomaliza masomo wanakuwa na ujuzi na kisomo wa kuchukua kupokea madaraka. Si unayaona majina yaliyopo kwenye uongozi wa Taifa?
    Na kuhusu TAIFA kupoteza ujuzi wa vijana, ni kweli, lakini uongozi ndiyo dili Bongo. Tunaona jamaa wote waliosoma na ujuzi mbali mbali wamekimbilia uongozi. Na bila hivoy mtu na elimu yake anweza kulala njaa na matajiri ambao hawajasoma nao wamekimbilia uongozi kwani wanajua bila uongozi jamaa walioko kwenye uongozi watawanyanyasa. Ukweli ni kwamba uzalendo Tanzania umekwisha na ukijaribu kufanya uzalendo na kuwa na utu unachekwa na kufedhuliwa.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Kwanza,

    Unalaumiwa na wengine humu lakini huo uliosema ni ukweli wa mambo.

    Watanzania tumeelekeza sana nguvu kwenye kutafuta Madaraka na Umaarufu badala ya kuchapa kazi na kujituma kwa mslashi ya Taifa na wananchi.

    Ukiona watu wanagombea uongozi bahati mbaya sana lengo lao lipo kwenye maslahi na umaarufu tu.

    Na mara zote tumekuwa tukigawanyika sana ktk mchakato wa kutafuta madaraka mfano kila baada ya Uchaguzi ni lazima patatokea mgawanyiko na mifarakano.

    Hivyo Mdau amesema ukweli kabisa na baya zaidi wengi wameelemea kwenye kujinufaisha na ubibafsi badala ya kutafuta Uongozi kwa faida ya wengi au ya wananchi wa kawaida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...