Timu ya Majimaji ya Songea imefanikiwa kujiwekea kibindoni jumla ya pointi 15 na hivyo kuamsha matumaini ya kupata nafasi ya kurejea ligi kuu ya soka Tanzania bara. Katika mchezo uliopita Majimaji imeidungua Polisi Iringa kwa jumla ya mabao 3-2. Majimaji bado Ina michezo mitatu ya nyumbani ambayo ikifanya vizuri yaweza kupata nafasi ya kurejea ligi kuu. Katika kundi lake tayari timu ya Mbeya City imejihakikishia nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao. Wapenzi kibao wa soka hapa Ruvuma wanaiombea Majimaji ipande daraja ili waufaidi uwanja wao wa nyumbani kwa kutazama ligi kuu ambayo wameimiss kwa miaka karibu mitano sasa. Pichani timu ya Majimaji ya Songea ikikaguliwa na Mgeni rasmi Kabla ya pambano lake dhidi ya Polisi Iringa.
Picha na mdau Gerson Msigwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...