Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka ( kulia) akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa Habari , Robat Dreyfuss wa Gazeti la The Nation la Marekani aliyefuatana na wabunge wa baraza la Congress ambao waliotembelea hivi karibuni ( Feb 21) wilayani Mvomero kuangalia shughuli za kimaendeleo ya wakulima wa zao la mpunga wa chama cha ushirika Dakawa kutokana na msaada wa fedha uliotolewa na nchi hiyo kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka watu wa Marekani ( USAID).
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( kushoto) akiteta jambo na Mgeni wake eneo la viwanja vya Ofisi ya Uwawakuda, Dakawa.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Anthony Mtaka ( kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa baraza la Congress la Marekani, John Garamendi ( kati kati ) akiwa na mwenzake Betty McCollum ,walipotembelea hivi karibuni ( Feb 21) wilayani Mvomero kuangalia shughuli za kimaendeleo ya wakulima wa zao la mpunga wa chama cha ushirika Dakawa kutokana na msaada wa kifedha wa nchi hiyo kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo kutoka watu wa Marekani ( USAID).
Baadhi ya wanaushirika wa kilimo cha umwagiliaji zao la mpunga, Bonde la Dakawa wakiimba nyimbo ya ukaribisho kwa wageni kutoka Marekani waliofika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( wapili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake wa kutoka Marekani eneo la Dakawa.
Ujumbe wa nchi ya Marekani wakisililiza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kilimo cha umwagiliaji Dakawa.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...