Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa akiongea katika hafla hiyo
Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa akitoa shahada ya heshima kwa waandaaji
Queense
Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la
New York ( City University of New York ) mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho sanaa za kitanzania.
Maonesho hayo
yaliyofanyika katika Chuo hicho
yanaelezwa na waandaji
ni ya kwanza kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani, yalipewa
jina la SHANGAA-Art of Tanzania likihusisha
mkusanyiko sanaa zaidi ya 112 lakini kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli kama
lilivyo jina la maonesho hayo,
ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo.
Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa ndiye aliyepamba maonesho hayo kama mgeni wa heshima, akiambatana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania
Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.
Sanaa
zilizopamba maonyesho hayo zilikuwa ni
za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika Mikoa ya Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa
na video zilizokuwa zikionyesha aina mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na
utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.
Jumla
ya sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa
wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza kuoneshwa kutokana na uhaba wa
nafasi.
Kwa
kutambua umuhimu wa maonyesho hayo
Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa waandaaji wa maonesho
hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...