SIKU MOJA baada ya Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake
katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo
eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar
es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko
huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi
wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya
jiji la Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la
ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na
maduka, makazi na Ofisi.

Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa
maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi
huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
hilo jengo likishakamilika tunasubiri ankali michuzi atuwekee hapa alafu aseme vingangua anga vinazidi kuongezeka jijini dar
ReplyDeletehahahaha vikwangua anga vinakuaga vimekaa vyema sana tatizo watanzania wengi ni masikini huko mikoani na vijijini sasa kujengeka kwa mji sioni kuwa ndio maendeleo ya taifa.