My dear Michuzi,

Greetings, napenda kumrekebisha mwandishi wa habari aliyeandika habari kwamba gharama za  kuunganisha umeme zilikuwa Sh milini mbili na sasa zimepunguzwa na kuwa sh laki nne na elfu arobaini. Hiyo si sahihi gharama halisi kwa sasa ni kama ifuatavyo;

Katika umbali usiozidi mita 30., 

Bei ya punguzo  itakuwa ni shilingi 99,000/- kwa umeme wa njia moja na tatu. Hii ni tofauti na bei ya zamani ambayo ilikuwa ni shilingi 455,104.76 kwa njia moja na 912,104.74 kwa njia tatu. 


Punguzo hili limetolewa na serikali ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi katika mikoa hiyo  wanapata huduma ya umeme ili kuharakisha maendeleo katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Badra Masoud

Msemaji TANESCO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mangi wa KiboshoFebruary 19, 2013

    Badra ni kwa Mtwara na Lindi tu au na Mikoa yote? Tunaomba ufafanuzi mama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...