Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Dk Sospeter Muhongo, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Uingereza kuanzia tarehe 25 hadi 28 Februari 2013.
Akiwa London Mhe. Waziri angependa kukutana na Watanzania waishio Uingereza kuzungumzia maendeleo ya sekta ya nishati na madini Tanzania na pia kubadilishana nao mawazo kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.
Ubalozi wa Tanzania, London unapenda kuwakaribisha watanzania siku ya Jumanne tarehe 26, Februari 2013, Ubalozini saa 11 Jioni. Anuani ya Ubalozi ni 3 Stratford Place, W1C 1AS, London
 Wote mnakaribishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wandugu mliopo UK hiyo ni nafasi muafaka.

    Mwelezeni Mhe. kuwa haya mambo mawili (2) hapo chini ni muhimu kurekebishwa ili twende na wakati.

    Kwa kuwa dhamira kubwa ni kuleta Tija ktk Sekta ya Nishati Serikali kupata faida pia na kuwafikia Wananchi kwa manufaa.

    1.Masoko ya Hisa kuwa wazi kwa kufungua,

    (i)T-Bonds and T-Bills (Dhamana za madeni kuweza kuwekezwa na wananchi wa kawaida badala ya Taasisi peke yake kama ilivyo sasa)

    (ii)Kuondoa Limit ya ununuzi wa Hisa usizidi 60% ktk Masoko, na pia kuwaruhusu Wageni (na Waliopo nje ya nchi kama ninyi Madiaspora) kuwekeza au kuwa Wadau ktk Soko huku Usimamizi makini ukiwepo.

    (iii)Kulifungua Soko liweze kufanya Biashara na nchi za nje, Cross border Trading Links, na kupanua wigo wake wa ufanisi ili kuakisi Mitaji ya nje zaidi.

    (iv)Kubadili Sheria zinazobana Uwekezaji na hasa kuingiza Sheria na kanuni za Kibiashara ktk Sekta ya Nishati (Energy Sector Commercial Laws)

    (v)Majukwa ya Uwekezaji (Investment Portifolio) yawe wazi kuruhusiwa kwa watu wananchi wa kawaida.
    KAMA INAVYOONEKANA SERIKALI INATAFUTA US$ 10 BILLION ILI KUPATA UWEZO WA KUJENGA MIUNDO MBINU NA VIWANDA VYA BIDHAA ZA GESI, WAKATI FEDHA KAMA HIYO INGEPATIKANA KWA NJIA KAMA HIZO HAPO JUU (i) na (ii) KUTOKA VYANZO VYA HUMU HUMU NCHINI BADLA YA KUKOPA KWA RIBA YA JUU KWENYE VYOMBO VYA NJE YA NCHI.

    2.Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Social Security) ndio njia muafaka kuwezesha faida ya Rasilimali kuwafikia Wananchi na kuondoa Umasikini nchini kwa kuanzisha Dhamana za Huru (Sovereign Bond), kama jinsi nchi za Norway,Oman na United Arab Emirates (UAE) zilivyo fanikiwa kuweka jamii zao nje ya Umasikini kwa Rasilimali za Nishati walizonazo (Oil and Gas,Energy Sector).

    Kama tunavyoona sasa Mifuko kama NSSF,GEPF na mingine imeweza kukuza wigo wake kuwafikia hata wananchi wa kawaida.

    ReplyDelete
  2. Hivi kama mawaziri wanakwenda kuonana na watanzania katika baadhi ya nchi hasa Uk. Hizi balozi zetu na wafanyakazi wake wanafanya nini kushindwa kuwakilisha serikali na nchi huko nje.
    Huyu mh. Prof mihongo anachoma kodi zetu kwenda kutalii London kwa kisingizio cha ajabu kabisa. Hizi ni kazi za mabalozi na si mawaziri kuacha afisi dar kwenda nje.
    Hiki ni kichekesho...kama ni nishati kwa nini asiende angalau Sauzi Afrika, korea, au UAE ambao wako safi tuuuu.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...