Na Maelezo Zanzibar
Mamia ya Wananchi wa Zanzibar leo wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwa kwa kupigwa Risasi na Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope Wilaya ya Kaskazini B,Unguja.
Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria.
Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na kuongeza kuwa itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikacana Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa watulivu bila kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake ili kuwabaini waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo.
Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo katika Kanisa la Minara Miwili Mjini Zanzibar.
Padri Mushi alifariki dunia Februari 17 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani kuendesha Misa ya Asubuhi katika Kigangwe cha Mtakatifu Teresia eneo la Beit El Raas mjini Unguja
Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani ambapo umauti ulimkuta akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya Jumapili ya kwanza ya Kwarezma.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara Miwili mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi.
Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,
Picha na Ramadhan Othman,IKULU.
tuache utani, sisi waislamu tunapenda uchokozi...inabidi tubadilike
ReplyDelete...leo tumemzika mwenzetu aliyeondoka kabla ya muda wake, Mungu amtangulie.
ReplyDeletemaswali mengi yanabaki:
Je Tanzania bado kuna nafasi ya kuishi kama ndugu hata kama hatukubaliani ki-imani?
Je jirani zangu waislamu (hapa Sinza) wananitambua kama mkiristo kwanza au kama mtanzania mwenzao kwanza??
Je tuko tayari(wote) kuwakemea kwa nguvu na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wachache wanaoleta uchochezi???
wacha utumbo utumbo wako wewe anonymous wa mwanzo na maneno yako ya uchochezi eti sisi waislamu tunapenda uchokozi,kwanza zanzibar unaijua historia ya wazanzibari na nchi yao usilete zako za kuleta hapa usione watu wameka kimya ukawaona wapuuzi na hawakwenda shule wewe tuliza ball tuna jua kila step za uchokozi wako na mungu ndo tunayemtegemea na fitna zenu na wala si muislamu wewe usitake kuwadanganya watu katika blog hii nenda zako ukooo kitimtim
ReplyDeleteLABDA WW NDO UNAPENDA UCHOKOZI. LAKINI MAJORITY NI WATU WA AMANI NA WANAPENDA UTULIVU. SO SPEAK FOR YOUR SELF
ReplyDeleteyoo michuzi na jamaa wote wadau wenzangu mlio wastaarabu wagwana na wenye kutumia hikma na busara hebu chekini hii commment ya jamaa hapo juu wa mwanzo mnaionaje na nani mchokozi na kweli mnahisi imetoka kwa muislamu hasa mwenye kuijua dini yake na uchungu na dini yake na nchi yake. kazi kwenu kuna watu wanajidai kujipachika pachika kama kweli mwembiyeni atoe jina lake na atuambiye uchokozi gani tulioo nao sisi waislamu na tulio ufanya zaidi yake aliyekuja hapa na unafiki wake.
ReplyDeletemwana saikologia ambaye nachukua shahada ya uzamizi(phd) nishakusoma mwanangu sana tuu na nisakuona una uchokozi wewe babangu nakushauri uwe mstaarabu ukituma comment zako hata kama shule hapandi si wakati wa kutuma comment za uchochezi poa moto baba usipo angalia utakuwakia mwenyewe mchimba kisima huingia mwenyewe
mdau majuuu na chini
Achomekae msalaba, si Muadhama Kardinali Pengo, ni Mhashamu askofu Agapit Ndorobo wa Jimbo la Mahenge
ReplyDeleteFixya. Uncle
Mie nadhani hapa si udini mbona tunakua vipofu kiasi hiki?yaani watu wanashindwa hata kufikiri au hata kuhusisha mlolongo wa matukia ili kuleta picha halisi ya hivi vitendo.Nionacho mimi hapa ni kwamba kwa kuendelea kuhusisha mambo haya yanayotokea na udini ndiko kutakapopelekea matatizo hayo ya udini kuanza,Nina hakika kifo hiki hakiusiani hata kidogo na udini, ni mambo mengine tofauti ambayo viongozi nao wanajitia hawayajui.SIO DINI JAMANI TUCHUNGUZE KWA MAKINI TUTAMJUA MMBAYA WETU SI PUNDE, VINGINEVYO TUTACHONGANISHWA NA KUUMIZANA WENYEWE KWA WENYEWE KWA KUTOKUA MAKINI KUMTAMBUA MMBAYA WETU.
ReplyDeletefabya uchunguzi wa kina hapa hapana muislam aliehusika na hichi kifo wewe mtoa mawazo wa kwanza tumia akili yako
ReplyDeletena wacha uchochezi wakijinga ...fumbafuuuuuuuuuuuuuwe
mmm jamani inaumiza, Kwa nini ??????? amewakosea nini?
ReplyDeleteemancipate yourselfs from mental slavery!!babylon has nailed it salaam kutoka texas hii mimi wa mombasa zanibar nimezaliwa na minara miwili napajua ...mungu tupe salama
ReplyDeleteWao wanapigana VITA ya 'nyama na damu' sie tunapigana vita ya kiroho na kamwe hawataweza kushinda vita ya kiroho kwani jemedari wetu yuu HAI hafi wala hajeruhiwi!
ReplyDeleteall in all wote tutasimama mbele ya hukumu ya munyezi Mungu subuhanah huwataallah bila kujalisha ukristo au uislamu kujibu tulichokitenda kama chema au kibaya.
ReplyDeleteInasikitisha Comments nyingi hapa ni za jazba, na zisizo na busara. Hata mwingine anadhiriki kusema "nina UHAKIKA kifo hiki si sababa ya dini..". Huyu hafai hata kuisaidia Polisi. Lugha zinazotumika hapa kupinga jazba zenyewe zina jazba! Sasa hii inadhihirisha nini?
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania
Kwa mungu hakuna dini, wala ubaguzi, kwa mtazamo wangu mtu yeyote mwenye dini lazima atakua mbaguzi, atajiona yeye ni bora kuliko wa dini nyingine, ingekua rahisi watu wote tusiwe na dini
ReplyDeleteMUNGU HAKAWII KULIPIZA KISASI KWANI NENO LAKE LINASEMA KISASI NI CHA KWAKE MWENYEWE. WE NDUGU UNAYETOA ROHO YA MWENZIO KUMBUKA NA YA KWAKO ITATOLEWA LABDA KWA NJIA MBAYA ZAIDI YA HIYO ULIYOTUMIA
ReplyDeleteHakuna kosa linalomruhusu binadamu kutoa uhai wake wala wa mtu mwingine. Haya ni matunda ya Uibilisi kwa upande wa wauwaji. Huwezi kuwa mtu mcha Mungu na kufanya mauwaji.
ReplyDeleteAcheni vyombo vya dola vifanye kazi yake....hakuna hata mmoja wenu mwenye jibu hapo...kilichobaki ni kuzidi kumuomba mwenyezi mungu atuepushe na majanga haya. Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. AMEN.
ReplyDeleteNi bora kuomba UN watuweke ktk Mpango wao wa DRONES pamoja na Mashariki ya Kongo.
ReplyDeleteIli kuondoa hali ya kuhisiana vibaya kati wa Waislamu na Wakristo nchini na kuondoa sintofahamu zozote ni Bora tukaomba UN ITUINGIZE KTK MPANGO WA HAYO MADEGE YASIYOKUWA NA MARUBANI KAMA WANAVYOPANGA KUULETA MPANGO HUO MASHARIKI YA KONGO ILI KUJUA NI NANI YUPO NYUMA YA MAPIGANO YASIYOISHA MASHARIKI YA KONGO!
Hivyo na sisi tutaweza kufahamu ni nani anahusika na mambo yanayo endelea nyuma ya pazia huko Zanzibar.
Ni jambo baya sana, tukaendelea kuishi kwa kuhisiana katika masuala mazito kama jinsi yalivyotokea mauaji huko Visiwani.
Hakuna mwenye uhakika alieweka comment hapo juu ni dini gani. Yeye mwenyewe ndie anajifahamu maana ndie alieweka. Hivyo kwa mtu yoyote mwenye hekima hana haja ya kuanza kugeuza mambo na kuhisi na kulazimisha hisia zake ziwe sahihi.
ReplyDeletemtu yeyote atakayejibu hoja "kwa jazba na taharuki" hatumii busara!na mtu akiguswa lazima atalipuka,kama hayakuhusu,vipi uwake? its a fools paradise! heri yao wale walioamua kukaa kimya , kwani kimya chao kina mshindo , kuliko wale waliamua kupwayuka ,wakilazimisha wasikilizwe , hata kile watakacho kisema kiwe kinawasuta nafsi zao!ukweli utabakia ukweli tu , hata ukipakwa rangi gani!na njia ya mwongo ni fupi!historia ya zanzibar niijuavyo miye , ni kwamba , babu zetu na bibi zetu walitekwa kutoka bara kwa kila hila zisizo mithilika , na waarabu ambao waliitumia dini waijuayo wao ili kuwarubuni , na hatimaye kuwageuza watumwa , na bila ya kujua wakafikishwa visiwani zanzibar na kupigwa mnada kama "mbuzi wa gulioni",waliobahatika kubaki zanzibar ndio hao waliozaliana hadi hii leo tuna washuhudia baadhi yao wakidharau asili yao!na walichukuliwa mateka hadi nchi za uarabuni na wengine mashariki ya mbali na magharibi ya mbali , historia yake ipo hadi hii leo!ushahidi upo na historia haifutiki!sasa kipi,huyu bwana anacho dhani watanzania hawakijui?
ReplyDeletetaratibu bwana mdogo au sijui bibiye because ni anonymous wa feb 21 at 11:45 am, eti warabu wamewafanya watu watumwa na kuwauza kama mbuzi je mzungu amekufanyeni nini? na mpaka hii leo anakufanyieni nini? soma historia baba uijue nenda marekani umulize mtu mweusi mkiristo mwenzako je mzungu ni mtu bora kwako kuliko muarabu?
ReplyDeletemtaa kaa hivyo hivyo kuwabudu wazungu wenu na na kuwaponda warabu lakini hakuna aliyeleta utumwa mbaya kama mzungu na bado mpaka hii leo mzungu anatumia psychology kuzichezeeni akili zenu na ndo maana mko majuha mpaka hii leo.
eti mungu wetu yuko hai, si mmesema yupo pamoja na bwana mbinguni si alikufa.
wananitai kinyaa nyaa watu wasio kwenda shule au wasio kuwa na akili za kufanya research na kujijua wao wanatafuata ya wenzao na dini zao ili kuwakashifu kumbe wanajikashifu wao wenyewe wasio na haya wasio jua vibaya, wasio na haya wanamjiwao nao uko tanganyika
ReplyDeleteKUNA AGENDA YA SIRI HAPA. HILI NI SUALA/TUKIO KUBWA NA NYETI SANA, MAISHA YA MTU YAMEPOTEA, KESI HAIJAANZA.
INAKUWAJE TUNAANZA KUONYESHEA VIDOLE UPANDE FULANI?
HII INAONYESHA WAZI KABISA KUWA WENGI WETU AKILI ZETU ZIMECHOTWA, MIND CONTROL INAFANYA KAZI.
TUSUBIRI TUTAUPATA UKWELI, DUNIANI HAKUNA SIRI. UTADANGANYA WATU KWA MUDA FULANI TU, HUWEZI KUWADANGANYA MUDA WOTE.
ReplyDeleteANON wa FEB 21st "mkweli"
Inawezekana huyo aliyetoa mada hiyo kuna kitu anajua na yuko na uhakika nacho.
Mwaka jana kuna Padri alipigwa risasi siku ya Xmas, yakajitokeza maneno yaliyoegemea upande mmoja. Baada ya muda kimyaa! Kumbe inasemekana alimtia mimba mke wa mtu.
Tufanye subira tutasikia tu, na ukweli utapatikana.