![]() |
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson |
Na Mwandishi Maalum
Wakati viongozi wakuu mbalimbali nchini Tanzania wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa
madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa
nao kwa upande wake unaeleza kwamba ni
kwa njia ya mazungumzo
migogoro ya dini inaweza kuepukika.
Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa, umetolewa na Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa chombo hicho ya kimataifa , wakati wa
tukio maalum la Muungano kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia
ya maelewano ya madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika
mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha wawakilishi kutoka dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali
na mabalozi.
“Migogoro mingi inayoendelea hivi sasa duniani, ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya
imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii. Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya
mazungumzo ili kujenga maelewano na
kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema Naibu Katibu Mkuu
Na kuongeza kuwa, dini zote
zimekuwa mstari wa mbele katika juhudi
si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.
Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu
na mateso katika jamii.
Na kwa sababu hiyo akasisitiza
kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali kuharibu na kuvuruga amani na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na
madhehebu ya dini .
“Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu wenye misimamo mikali kuharibu kazi nzuri zinazofanywa na jumuia za kidini kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson
Akaelezea wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa na vikundi vyenye misimamo mikali
kueneza kampeni za chuki na vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu
ili wao watimize malengo yao.
“Kwa kawaida vijana wana nguvu. Tunapashwa
kutafuta njia nzuri na sahihi za
kuwafanya wazitumie nvugu zao kuboresha
maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Naye
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa upande wake alisema Umoja wa Mataifa unaweza kufaidika sana kama viongozi wote wa dini watajihusisha na
kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na
madhehebu ya dini.
“ Hebu basi na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani
zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana
wenyewe kwa wenyewe,ikiwa ni pamoja na
uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti
zetu za imani”.
Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila
mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya
kwamba kama vyanzo vilivyopita vya
migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya
kuitumbukiza dunia katika machafuko ya
kutisha.
Hakuna migogoro ya kidini. Ingekuwepo, watu wangekuwa wanagombania usahihi wa imani zao na hapo kungekuwa na migogoro zaidi ndani dini zenyewe. Kilichopo ni Biashara tu, migogoro ina faida kubwa kwa baadhi ya vyama, taasisi za kiraia, kidini au watu binafsi. Ujinga wa waumini unatumika tu. Ndiyo, dini imegeuka biashara na migogoro ni kama matangazo ya hizo biashara.
ReplyDeleteHatuwaamini hawa wazungu. Ndo maana walimuondoa Dr. Asha Rose Migiro. Wanataka waafrika tuamini kuwa migogoro ya kidini ndo tatizo badala ya "unequal distribution of wealth". Wao wazungu wanaendelea kutunyonya. Matabaka ya kiuchumi ndo yanaleta migogoro wala si kitu kingine na wao hili hawataki kulikubali ili waendelee kututawala. Wanajifanya kuwa vurugu za Afrika zinasababishwa na udini na ukabila. Kwani udini na ukabila unaletwa na nini kama si umasikini unaochangiwa kwa kiwango kikubwa na wazungu wenyewe? Mdau-CA, USA
ReplyDelete