Tembo Architects imetangaza kuwa kampuni hiyo imechaguliwa kusanifu jengo isiyofanana na lolote lile kaskazini mwa Tanzania. Mradi huu utamuweka katika ramani ya dunia Mike Tembo ambaye ni mbunifu anaeongoza. Mradi huu ni wa kwanza kwa Tembo kufanya kijijini, Tanzania.
Jengo hili litakalojengwa katika eneo ambalo bado halijatajwa kaskazini mwa Tanzania limefadhiliwa na tajiri mmiliki majengo toka Afrika Kusini, Nicholas Van De Kaamp. Akiwa maarufu kwa ujengaji wake wa nyumba na kuziuza kwa wananchi kwa kiasi kisichozidi 10,000 ZAR, mwanzilishi huyu inasemekana atauza nyumba vya jengo hili kwa wananchi wa kipato cha wastani.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Tembo, Van De Kaamp na mradi huu unaokuja tembelea tovuti hii: http://bit.ly/XIZ02p
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...