Afia mtendaji mkuu akifungua mdahalo wa Jinsia kwa Maendeleo uliofanyika Kilwa Masoko na kuendeshwa  na Mtandao wa Asasi ya Kingonet chini ya Ufadhili wa The Foundation for civil Society.
 Wadau mbalimbali waliohudhuria mdahalo wa Jinsia na Maendeleo uliofanyika wilani Kilwa jana
 =======  ======= ======

Na Abdulaziz,Lindi.

Imeelezwa kuwa Baadhi ya mila na desturi  zilizopitwa  na wakati
ambazo zinaendelezwa hivi sasa zinachangia kwa kiasi kikubwa tabia ya unyanyasaji  wa kijinsia ikiwemo ya ushirikishwaji  watoto wa kike kwenye vikao vya kifamilia vinavyojadili ndoa na Talaka ikiwa pamoja na kuchangia maamuzi Pamoja na kila jamii kuzingatia ,kulinda na kudumisha mila na desturi zake  lakini kuna haja ya kuzichambua  upya ili kuzipata zile nzuri
zinazofaa kwa  na kuhakikisha zile zinazokandamiza wanawake
zinatokomezwa.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Masoko wilayani Kilwa,Bw Peter Amos Malekela alipokuwa akifunga na
kufungua katika Midahalo miwili iliyofanywa katika Jimbo la Kilwa
kusini na Kilwa kaskazini iliyoendeshwa na Mtandao Mwavuli wa Asasi
zisizo za Kiserikali Wilayani Kilwa (Kingonet) Malekela aliwataka wanawake kuachana na mila hizo kandamizi na badala yake wajitokeze kufanya kazi  za maendeleo ikiwemo kugombea nafasi mbalimbali masuala ya siasa  ili wawe miongoni mwa viongozi wa kufanya maamuzi  mbalimbali katika maeneo yao.

“Mafanikio yoyote  mwanamke  ndiye anastaili  kupongezwa kutokana na
jukumu alilonalo katika familia, hivyo ni vyema taasisi za  mbalimbali
 na wadau wa maendeleo  na wana siasa wakawaonyesha wanawake njia za
kuleta mbadiliko katika familia na taifa kwa ujumla’.Alimalizia
Malekela.

Awali akitoa maelezo mafupi ya Mdahalo huo,Katibu Mtendaji wa
Kingonet,Omary Mkuwili alieleza kuwa Asasi yake ipo kwa ajili ya kutoa
elimu mbalimbali kupitia midahalo kwa Lengo la kufikisha elimu na
kupokea Mawazo mbalimbali kwa wasiopewa nafasi kusikika  ili kuchangia
maendeleo ya Kilwa na Mkoa wa Lindi.

Aidha aliwaasa Washiriki wa Mdahalo huo kuachana na Imani zilizo
potofu za kujenga akilini kuwa Mwanamke akifanikiwa katika maisha
wanadhani  yupo mwanaume nyuma yake  amemwezesha mafanikio hayo lakini hapana wapo wanawake mwenye uwezo wa kiakili, mali na utendaji kuliko wanaume huku akibainisha kwa kiasi kikubwa  ndio viongozi  na washauri wakuu kujenga utamaduni na kusisitiza  kusaidia na kuchangia shughuli za  kuwajengea uwezo wanawake  ili kuharakisha maendeleo.

Midahalo Hiyo miwili iliyofanyika katika Kata ya Chumo na Kilwa Masoko
ikiwa na lengo la kujadili suala la jinsia inavyochangia maendeleo na
kuendeshwa na  mtandao wa mashirika yasiyo kuwa yakiserikali wilaya
Kilwa(KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for the civil Society.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...