Naibu mkuu wa pili wa Idhaa za Kiswahili wa DW, Josephat Charo. akimpa mkono wa heri kwa furaha Mtangazaji Stumai George baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja kuhudumu kama mtangazaji DW.
Stumai George akipewa mazagazaga na kulambishwa nondo ya bye bye mama lakini uwe unakumbuka DW na Naibu mkuu wa pili wa Idhaa za Kiswahili wa DW, Josephat Charo mjini Bonn.
Wafanyakazi wa DW katika hafla fupi ya kwa heri ya kuonana Stumai George ambae anarudi Star TV Dar es Salaam.
Wafanyakayi wa DW na Kicheko kinachoashiria dhahiri kwamba Stumai George pamoja na kuondoka lakini mwenzao wa dhati.
WANZAAGWA KUTOKA NCHI GANI KURUDI TZ?
ReplyDeleteMdau huyo Mtangazaji anaagwa kutoka nchini Ujerumani kurudi Tanzania.
ReplyDeleteStumai George baada ya mwaka mmoja wa kula ma-Hamburg na junk foods sasa karibu tanzania ili ule:
ReplyDelete1-Ugali wa dona kwa mbaazi kavu,
2-Ugali kwa matembele,
3-Dona kwa Kisamvu mchanganyiko na kunde mbichi,
4-Ugali kwa Dagaa la Kigoma,
5-Mchanyato wa maboga, maharage mabichi na viazi kwa maziwa ya mtindi,
6-Wali chuku chuku kwa samaki ndobe,
7-Makande kwa Kachumbari(Biriani Pori)
Nadhani Menu hiyo hapo juu itawajaza mate ya makoo wa Majuu au siyo?
hahahaha mdau watatu,
ReplyDeleteBibie Mtangazaji baada ya miziki ya kujiandaa kulala, hadi miziki ya wakati wa kula chakula ukiwa huko Majuu karibu Tanzania:
-ucheze lizombe,-Kingoni.
-echeze mdumange,-Kisambaa.
-ucheze ndalandala,-Kimatumbi.
-ucheze tokomile,-Kindengereko.
-ucheze behobeho,-Kikwele.
-ucheze mbeta,-Kiluguru.
-ucheze mganda,-Kinyasa/Kiyao.
!!!!!!!
DW msitupe jongoo na mti wake,
ReplyDeleteMtowe na mialiko ya mara kwa mara ili mdau mtangazaji abadilishane nanyi ujuzi na maendeleo, msibane kwa sana sasa...sio mara ohhh, Bajeti kutoka Bungeni Bundestag-Berlin safari hii hakuna fungu la kutosha!...mara ohhh, matumizi ya wageni wa nje yamepunguzwa!
Wabaki hao Ubalozi pekee hapa Dar na sio ninyi tena!
mbona simuoni hapo Abuubakar Liongo...mzee wa yaliojiri?
ReplyDeleteJirupue au kama ulikuwa na akili ulikuwa utafute dume likuzalishe. Rudi mama mkataa kwao mchawi.
ReplyDeleteHaaaaa umeniu na hiyo menu yako,,,1
ReplyDeletebasi ujue majuu tena hapa Ujeru' kumejaa ma-Afro shop kibao....kambale...sato...mchicha...bamia, ngogwe vimejaa kwa wingi....Utumbo fresssh...alafu juzi nimepika kongoro!1 menu ya leo kuna mkia mzima wa n'gombe hapa sasa sijui kama nitamaliza. Unakula ukiwa bongo ndo unazidisha hasira ya kuzichanga...haaaaaa
Mate ya kinywa bwana siyo ya makoo, koo haliweki mate ya kutamanisha vyakula, huweka ya kikohozi. Ila siyo siri, kweli hiyo MENU inatamanisha.
ReplyDeleteMbona simuoni cheupe a.k.a WHITE?
ReplyDeleteAu alienda K.F.C? bwahahaaa!
Au anahuzunika Stumai kuondoka?