MNAMO TAREHE 12.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NDANI YA NYUMBA YAKE.

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA KIUNGO HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA ANAKIRI KUMILIKI KIUNGO HICHO AMBACHO ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA KIENYEJI KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA NA FEDHA ZAKE. 

 TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO KWA BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO. 

 AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA KUUCHUKIA UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA UNAOJITOKEZA KATIKA MAENEO YAO. 
 Signed by 
[B.N.MASAKI -SSP] 
KAIMU KAMANDA WA POLISI MBEYA
BARAKA KIBONA, MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU HAPA AKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
MTUHUMIWA AKIPAKIWA NDANI YA GARI YA POLISI

HAYA MABOKSI INNASADIKIWA YALITAKIWA YAJAE HELA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA ILOLO WAKISHANGAA TUKIO HILO NYUMBANI ALIKOPANGA MTUHUMIWA HUYO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. jamaa amekutwa na kiganja (ouch), mwingine kwenye hiyo picha juu hana kichwa lakini amesimama, mji una washirikina wa kumwaga.

    ReplyDelete
  2. Kwanza inasikitisha, halafu inatia aibu, lakini njaa haina adabu, eti uweke kiganja kwenye boksi halafu maboksi mengine yote yatazaa mahela, basi wananchi wote wataishiwa viganja, watu wangegeuka fisi, mtu upo matembezini mzali anakunyemelea na kukata kiganja kwa kisu kikali, Mungu tunusuru watanzania, tufungue macho yetu yenye ukungu and matongo tongo tuweze kuoan bayana, na tuachana na ushirikina.

    ReplyDelete
  3. wewe anony wa kwanza nini wewe!unashangaa jamaa kusimama bila kichwa. Mbona jamaa wengine wanasimama bila miguu. Acha kutuzinguwa.

    ReplyDelete
  4. Mangi wa KiboshoFebruary 14, 2013

    Mbeya ina makanisa ya ajabu kama NIgeria na ndio inaongoza kwa mambo ya ushirikina TZ.Wanyakyusa, Wafipa na Waswafa Mrudieni Mungu wa kweli jamani!

    ReplyDelete
  5. Huyu ameonewa...mbona waTZ wengi kuanzia vigogo mpaka vishina ni ushirikina mtupu.

    Hii ndio mila ya waTZ,aachiwe huyo anaendeleza mila

    ReplyDelete
  6. Sioni ajabu kwa taifa hili la kishirikina.Kama serikali iliamua kuhalalisha rufani ya watu wake walio wagonjwa kuhamia LOLIONDO kwa BABU MSHIRIKINA natukashuhudia viongozi wakubwa sana na walio tumaini la watu wote wakinyweshwa MAJI MACHAFU kwanini iwe tabu kumuajiri huyu jamaa pale BOT atujazie hazina yetu minoti?..Taka usitake HAPO NDIPO TULIPO.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa kwanza, anony wa Wed Feb 13, 09:26:00 pm 2013

    Hahahahahahaa!

    Huo ni muonekano wa picha kwa upande wa pili!

    Hiyo picha imepigwa upande wa pili ambako kuna kitu kinaning'inia kutokea juu kilipofungwa!

    Hivyo inaonekana kama vile jamaa aliyesimama upande wa pili hana kichwa!

    ReplyDelete
  8. Ohhh hawa Waganga watu wabaya sanaa!

    Ni kiasi cha kutumia akili tu!

    Sasa wewe Kijana Baraka Kibona, huyo Mganga kama angekuwa na uwezo wa kujaza Noti hayo maboksi yote angekupa wewe badala ya kujipa Utajiri yeye mwenyewe?

    ReplyDelete
  9. Baraka Kibona,

    1.Fedha hutafutwa kwa bidii maarifa na ubunifu, na sio kwa msaada wa kiganja cha mkono cha binaadamu mwenzio, ambae uwezekano mkubwa atakuwa tayari ni marehemu!

    2.Fedha ukiiweka Benki hakuna wa kuichukua hata awe Chuma ulete wa namna gani?

    ReplyDelete
  10. Tunahitaji kufanya mapinduzi makubwa kwenye elimu ili kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la imani za ushirikina au imani zozote zingine za zilizo potofu. Jamii iliyoielimika haitakuwa na muda wa kuhangaika kukata mikono ya watu wengine ili mtu awe tajiri au kukata viungo vya maalbino - Elimu pekee ndio mwanga ukaomulika giza lilijaa vichwani mwa watanzania wengi

    ReplyDelete
  11. Watu wenye mawazo mafupi na waliokata tamaa wawekewe kliniki ya kuwazundua kutoka imani hizi za kizushi. Ttz hata dini zingine zinaendekeza mambo haya na kuwajaza watu uoga.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa tatu na wa sita, loosen up a bit guys, just wrote the post for a joke! it is obvious that the hanging garment obscured the man`s head!
    Mdau wa kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...