Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa, amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.

Akizungumza hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.

``Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya, nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.

Katika fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam kwenye eneo hilo.

Ujumbe huo uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli, kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi.
ujumbe wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindikizawajumbe hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. duh kumbe hapo monduli mi nilidhani ostabei

    ReplyDelete
  2. Ndugu mwandishi wa habari hii, unapoandika habari yako tafadhali hakikisha unaandika ukiwa na uhakika nayo, siyo kuandika tu ovyo ovyo. Mimi ni mkaazi wa Buseresere na siyo Buserere kama ulivyodai wewe rafiki yangu, ninacholalamikia hapa ni wewe kudai kuwa mchungaji aliyeuawa ni wa kanisa la "kisabato", kuwa mwangalifu ndugu yangu kabla hujataka kuandika hususa ni kwenye mambo sensitive kama haya. Pia Mheshimiwa E.Lowasa nampongeza sana kwa kututaka watanzania akiwemo na yeye tumuogope Mungu na viongozi wetu wa Dini washirikiane kutegua "mtego" huu. Napenda kukujulisha kuwa suala hili lina mtego wa kisiasa tena kwa sehemu kubwa kwa sisi tulioko hapa tunajua, yote haya yanasababishwa na "peoples power" ambao wamekuwa wakiweka mitego mingi kama vile "mitego ya gesi Mtwara,

    ReplyDelete
  3. Hawa Jamaa (people's power) ITIKADI yao haikubaliki kabisa hapa nchini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...