Waandaaji
wa Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kutoa zawadi nono kwa
wanariadha watakaoshiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.
George
Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager alisema katika
taarifa kwa vyombo vyua habari jana kuwa“Kilimanjaro Premium Lager
inaendelea kutambua mchango wa wanariadha kwa kuwazawadia kwa mara
nyingine na mara hii ikiwa ni zawadi nono pamoja na motisha nyingine’’.
Alisema
fedha kwa ajili ya zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pande zote
mbili wanaume na wanawake kwenye Kilimanjaro Marathon kilometa 42 ni
zaidi ya shilingi milioni ishirini.
Washindi
wa kwanza wa Kilimanjaro Marathon kilometa 42 upande wa wanaume na
wanawake watajishindia Tsh Milioni 3 kila mmoja, lengo likiwa kuvutia
wanariadha wa hadhi ya juu duniani, kuhamasisha uwekaji wa rekodi mpya
na pia kusheherekea miaka kumi na moja ya Kilimanjaro Marathon.
Aliongeza
kuwa ‘‘Kipaumbele cha Kilimanjaro Premium lager ni kuwapa motisha
wanariadha wa Tanzania zaidi, na kwa sababu hiyo Kilimanjaro Premium
Lager wametenga kiasi cha pembeni cha Tsh milioni 6 kwa wanariadha
watanzania ambao watamaliza wa kwanza katika pande zote mbili wanaume na
wanawake katika mbio ya Kilimanjaro Marathon kilometa 42 kila mmoja
akijipatia milioni 3.
Kiasi
hicho cha fedha kitakabidhiwa kwa wanariadha Watanzania kama nyongeza
ya kile watakachopata kwenye ushindi wa mbio walizoshiriki na kushinda.
“Tunaamini kuwa hii itawahamasisha wanariadha watanzania kuongeza juhudi
na kumaliza mbio kwa muda mzuri”.
Washindi
wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja na wa washindi wa
tatu watajipatia shilingi 850,000 kila mmoja kwa wanawake na wanaume.
John
Addison, Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers ambao ni waandaaji wa
tukio hilo alisema Mshindi wa nusu Marathon kwa wanaume na wanawake
atajishindia Tsh 1,500,000 kila mmoja, mshindi wa pili Tsh 750,000 na
mshindi wa tatu Tsh 375,000.
Washindi
wa mbio za GAPCO Nusu Marathon kwa walemavu watajipatia zawadi nono
pia, ambapo mbio hizi zinajumuisha sehemu tatu yaani kiti cha matairi,
hand cycle na walemavu wengine na kila mshindi kwenye kipengele chake
atapata zawadi kama ifuatavyo;
Mshindi
wa kwanza Tsh 300,000, mshindi wa pili kwa wanaume na wanawake Tsh
200,000, na mwisho mshindi wa tatu atajinyakulia Tsh 50,000.
Kwa
upande wa mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run washiriki wote
watakaomaliza mbio hawataondoka mikono mitupu bali watajipatia t-shirts
na zawadi nyingine nono kama simu na muda wa maongezi pia zitatolewa
kupitia bahati nasibu. Mbio hizi ndio zinazotoa fursa kwa watu wa rika
zote kuwa sehemu ya Kilimanjaro Marathon.
Mbio
hizo zinaratibiwa na Executive Solutions na kudhaminiwa na Kilimanjaro
PremiumLager, huku wadhamini wengine wa tukio hilo ni pamoja na Vodacom
Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon Walemavu), Tanga Cement,
CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New
Arusha Hoteli, Kilimanjaro Water, FastJet na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Idadi ya Watu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...