Mheshimiwa Mathias Chikawe (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria leo amekutana na viongozi mbalimbali kwa nyakati tofauti na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo Wizara ya Katiba na Sheria inashughulika nao.
Mheshimiwa
Chikawe pia amefanya mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bw Johnny
Flentoe ambaye alimtembelea Waziri Ofisini kwake. Katika mazungumzo yao
wameongelea ziara wa Waziri Mkuu wa Denmark itakayofanyika hivi karibuni na
kuongelea mahusiano ya Denmark na Serikali katika nyanja mbalimbali. Mhe
Chikawe aliishukuru Serikali ya Kifalme ya Denmark kwa kuwa mdau Mkubwa wa
Sekta ya Sheria Nchini na kwa misaada yao kupitia Shirika lake la Maendeleo ya
Kimataifa la DANIDA katika Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria Nchini.
Misaada yao imefanikisha kuboresha miundombinu ya taasisi za kisheria na
kujenga mifumo imara ya sheria na kupanua wigo wa fursa za wananchi kupata
haki.
Mhe.
Chikawe akiwa kwenye picha ya pamoja na Lord Dholakia (kushoto) na Bw Julian
Chandler (Naibu Balozi wa Uingereza Nchini) mara baada ya kufanya mazungumzo
ofisini kwa Waziri
Mheshimiwa Chikawe amefanya mazungumzo na Lord
Navnit Dholakia ambaye ni Naibu Kiongozi wa chama cha Liberal Democrats cha
Uingereza na mjumbe wa All Party Parliamentary Group ambalo linajihusisha na
kufutwa kwa adhabu ya kifo. Lord Dholakia yuko nchini kwa ziara ya kikazi na
moja ya mambo aliyozungumza na Mhe. Chikawe ni mustakabali wa adhabu ya kifo
Nchini na kushauri kuwa wakati umefika kwa Serikali ya Tanzania kuangalia
umuhimu wa kuwepo au kutowepo kwa adhabu ya kifo na ameshauri uwezekano wa adhabu
hiyo kufutwa. Kwa upande wake pamoja na mambo mengine Mhe Chikawe
amemuhakikishaia Lord Dholakia kuwa kupitia
Mhe
Chikawe akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Bongani Majola ambaye ni Msajili wa
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari (ICTR
Waziri Chikawe pia
amefanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda (ICTR) Bw. Bongani Majola ambaye alimtembelea Ofisini kwake leo, lengo
likiwa ni kujitambulisha na na kuongelea shughuli mbalimbali za Mahakama,
mafanikio na changamoto za Mahakama hiyo. Mhe Chikawe amemuhakikishia Msajili
huyo kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na Mahakama hiyo na kumuomba
wawe tayari kusaidia pale ambapo sekta ya sheria itaona inahitaji msaada. Picha na Charles Joseph Mmbando
Suti nyingine zinafiti..lakini huwa ni kwa ajili ya Tall people!
ReplyDelete