Familia ya hayati Browne Charles Nindi na Fatma Nindi ya jijini Tanga,wanapenda kutoa shukrani zao dhati kwa wale wote walioshiriki pamoja nasi katika kumuuguza mpaka kumpumzisha
mpendwa wetu Charles Browne Nindi.
Charles alifariki Nov 6 2012 na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele Nov 10 2012.

Shukrani za pekee ziende kwa marafiki, majirani na madaktari wa hospitali ya Bombo jijini Tanga.Tunasema ASANTENI sana kwa faraja mliyotupa.
Kutakuwa na misa ya shukrani itakayofanyika Jumamosi tarehe 23 Februari 2013  katika kanisa la Anglican Kawe, Dar es Salaam Tanzania saa 3(tatu) asubuhi na kufuatiwa na chakula cha pamoja saa 7 mchana nyumbani kwa James Nindi.(0714 686 686)

                           Wote mnakaribishwa
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa. Wajuzi nijibuni,hivi neno hayati linatumika vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...