Mrisho Mpoto akiigiza kama FALSTAFF na kulia ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huu kwa Kiswahili, akicheza kama Bi Quickly. 
 Mrisho Mpoto akiwa na waigizaji wenzake kutoka Kenya ambao waliigiza kama WANAWAKE WA HERI WA WINSA  wakionesha umahiri wao katika Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Kulia kabisa ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huo kwa Kiswahili, akiigiza na wenzake huku akiwa kwenye husika nyingine.



Mrisho Mpoto ni moja kati ya wasanii wakubwa wa Muziki na Maigizo ya Jukwani hapa nchini. Michezo hii ya jukwaani ambayo ni adimu na adhimu sana hapa nchini kutokana na umakini na utaalaam mkubwa unao hitajika katika uandishi, uongozaji na hata uchezaji jukwaani.

Hapa nchini kuna wasanii wachache wenye uwezo wa kutimiza hatua zote za maandalizi ya mchezo wa jukwaani. Tumekuwa tukishuhudia  wataalam walio pikwa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo na wale wa Chuo kikuu cha Mlimani katika Idara ya Sanaa na Maonesho na Chuo kikuu Huria wakishughulika sana na tasnia hii.

Baada ya kuona Tasnia hii inasua sua, Bwana Mrisho Mpoto aliamua kwa dhati kurudisha heshima ya michezo hiyo kwa kuishawishi kampuni inayo jishughulisha na Maonesho ya Jukwaani ya nchini Kenya Kuuleta mchezo ulio jipatia umaarufu mkubwa kwenye nchi mbali mbali ulimwenguni na hata kupata heshima ya nyota tano nchini Uingereza ambapo Mrisho yeye mwenyewe akiucheza mchezo huo kama mhusika mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...