ANKO HABARI,
NIMEPANDA DALADALA ASUBUHI HII KUTOKEA KONGOWE KWENDA TANDIKA, SIKUPATA KITI. NILIMWOMBA MWANAFUNZI MMOJA ANISHIKIE MFUKO WANGU UKIWA NA VITABU. NILIPOFIKA MTONI KWA AZIZI ALI, NIKASHUKA NA KUSAHAU KUUCHUKUA MFUKO HUO,NILIPOHAMAKI GARI TAYARI LIMESHAONDOKA NA BAHATI MBAYA ZAIDI KONDA HAKUTOA TIKETI.
MWANAFUNZI ALIVAA SARE KAMA YA WAILES SEKONDARI. NIMEENDA PALE HAKUWEZA KUPATIKANA.
VITABU VIKO VITANO:
1.FROM GOOD TO GREATNAOMBA KAMA MWANAFUNZI HUYO ATAKUWA HANA NAMNA YA KUNIPATA BASI AWASILIANE NAMI KWA NAMBA 0755877827 AU0767626929
Kwanza pole kwa kupoteza vitu vyamtu. na huo ni ujinga mkubwa kila siku hayo mambo yanaongelewa. huwezi kumpa kitu mtu hajui ndani kuna nini na ni mwanafunzi. ati akushikie hayo nimakosa yako. watu wanatapeliwa namna hiyo ndani ya madaladala kilasiku. nishawahi kusoma humuhumu.na wewe unafanya tena makosa. tena wewe unapaswa ulipe haraka dhamana ya watu.
ReplyDeleteHiyo sio uzembe bali ni kupitiwa au teseme ubinaadamu.
ReplyDeleteJamaa ameomba asaidiwe kubeba huku akiwa hajapata kiti ndani ya basi, hivyo aloposhuka hakukumbuka kama alipanda na mzigo.
Pole sana ndugu E.Msangi!
wewe mtoa maoni wa kwanza,ninashaka kama unaongea ukiwa hapa nchini,mazingira ya usafiri wa hapa bongo ndiyo yanatufanya tuombane misaada ya kubebeana mizigo ndani ya daladala,inafikia hata wakati watu wazima wanapitia madirishani,hapa si ujinga ni ubinadamu tu,ingekuwa ujinga michuzi issa asingekubari kuweka jambo la ujinga hapa,hii ni blog ya jamii si yakijinga kama unavyofikiria.
ReplyDeleteNinashaka kubwa sana na uelewa wako wa mambo nakuomba sana usiwe unakurupuka kutoa maoni bila kuyatafakari,huyu mtu kapoteza vitu vyake,anaomba msaada kwa jamii imsaidie kama inawezekana na harazimishi mtu ,wewe unamwona mjinga. Kama ulivyomwita mwenzio mjinga kwa kuomba msaada,kunasiku litakupata jambo na utahitaji msaada kwa watu ndipo utakapo jua uliyoyaongea.Nakuombea maisha marefu yenye mafanikio sana ili uendelee kuita watu wajinga.AMEN