Na Mwandishi wetu, Shinyanga
Benki ya Afrika Tanzania imemwagiwa sifa na serikali kwa kutekeleza sera kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanapata huduma za kibenki kwa maendeleo yao na ustawi wa uchumi nchini.
Sifa hizi zimetolewa na waziri wa fedha, Dkt. William Mgimwa alipokua akifungua rasmi tawi la benki hiyo katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga jana.
“Tunawapongeza sana kwa juhudi zenu kuhakikisha kuwa mnatoa huduma kwa watanzania wengi kadiri inavyowezekana…hii ni nia ya serikali…asanteni sana,” alisema Dkt. Mgimwa.
Waziri huyo alisema kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja wa idadi ya benki katika nchi na kukua kwa uchumi na hivyo kutoa wito kwa vyombo vingine vya fedha nchini kuiga mfano wa Benki ya Afrika Tanzania kujitanua nchini pote.
“Nchi zote zenye uchumi imara zina msingi mzuri wa vyombo vya fedha kama benki,” alisema na kuongeza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira bora kuhakikisha kuwa huduma za kifedha kwa wananchi zinaimarika.
Hata hivyo, alitoa changamoto kwa mabenki hapa nchini kujitahidi kushusha riba kuwezesha wananchi kukopa na kurudisha mikopo kwa urahisi na hivyo kupanua biashara zao.
“Hii itawawezesha kukua kiuchumi na kujenga uaminifu,” alisema na kuongeza kuwa lazima wateja wa benki wajenge nidhamu ya kurudisha mikopo kwa wakati kuruhusu biashara kufanyika kama inavyotakiwa na bila matatizo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Balozi Fulgence Kazaura alisema mtandao wa benki hiyo katika nchi 15 barani Afrika iwe kichocheo kwa wafanyabiashara hapa nchini kutumia fursa hiyo kujipanua kibiashara.
“Wafanyabiashara hapa nchini watumie mtandao mkubwa wa benki hii kujitanua kimataifa,” alisema.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo katika benki hiyo, Bi. Mwanahiba Mzee alisema wananchi wa Kahama watarajie huduma za kipekee kutoka benki hiyo.
“Tutatoa huduma nzuri na za kipekee…huu ni wakati wenu kunufaika na benki hii,” alisema.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Bw. Benson Mpesya alitoa shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kwa uamuzi wa kufungua tawi katika wilaya yake.
Alisema wilaya hiyo ina shughuli nyingi za uchumi kama madini na kilimo ambapo alisema wanahitaji huduma nyingi zaidi za kibenki.
Tawi la Kahama linakua la 18 kufunguliwa na benki hiyo.
Tangu ianze shughuli zake hapa nchini, benki hii imekua ikijitahidi kujitanua kwa kuanzisha huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufungua matawi mapya.
Hadi sasa ina matawi kumi jijini Dar es Salaam pamoja na mengine nane katika mikoa ya Morogoro, Tunduma, Mwanza, Moshi, Mbeya, Mtibwa, Arusha na sasa Kahama.
Benki hii ni moja ya mtandao wa kibenki unaofanya kazi katika nchi 15 ambazo ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Ghana, Ivory Coast, Mali, Niger na Senegal. Nyingine ni Burundi, Djibouti, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.
Pia ina tawi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa akisisitiza
jambo kwa waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Benki ya
Afrika Tanzania wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga jana.
Waziri
wa Fedha, Dkt. William Mgimwa akiongea wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la
Benki ya Afrika Tanzania wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga jana. Wengine katika picha ni Mkurugenzi
Mwendeshaji wa benki hiyo, Bw. Ammish Owusu (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa benki hiyo, Balozi Fulgence Kazaura (kulia).
safi sana ccm oyeeee ankali michuzi oyeeee ok
ReplyDeletetunaomba tutundikie bei za madafu wadau tupange maisha vizuri.
asante
ccm oyeeee...
NAOMBA MWAKUMBUKE WANANCHI WANAOISHI KIJIJINI MAANA HAO NDO WANACHANGIA KUKUA KIUCHUMI NCHINI USUSA WILAYANI KAHAMA
ReplyDeleteNI ESAU LUGEMBE ,
KAHUNDA STATIONARY
BOMA ;ROAD,
KAHAMA