Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...