Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mhe. Leonidas Gama (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mzee Israel Elinewinga aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini zikiwemo za uwaziri katika Serikali ya awamu ya kwanza ambaye alikuwa amelazwa hospitali teule ya machame na kuruhusiwa mapema wiki iliyopita akisumbuliwa na maradhi mablimbali yakiwemo ya miguu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mhe. Leonidas Gama alimsaidia Mzee Israel Elinewinga kuingia sebuleni kwa kutumia kiti cha magurudumu.
Mzee Israel Elinewinga akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kilimanjaro waliofika nyumbani kwake kumjulia hali.
Mungu bwana hamtupi mja wake, huyu mzee wakati akiwa waziri wa elimu alihakikisha umeme unaenda Masama kupitia milimani juu ndio uteremke kwa sadala matokeo yake kila mmoja alifaidi.Pia elimu iliboreka sana na hakusahau nyumbani kwani msahau kwao mtumwa. Viongozi wa leo wakiiba wanaenda kuwekeza South africa na Dubai. Angalia hata yeye pamoja na uzee na kustaafu yuko mahala bomba wengine huwa hata aibu kuonesha wanakolala. Viongozi mtavuna mlichopanda, ukipanda maendeleo utavuna maendeleo ukipand aufisadi na wizi utavuna aibu na fedhea.
ReplyDelete