Picha ya pamoja baina ya Ujumbe wa Bunge la Tanzania na uongozi wa Majlis Dawla ndani ya ukumbi wa Bunge hilo Muscat Oman.
Naibu Spika Mhe.Job Ndugai akiongoza ujumbe wake katika mazungumzo na Uongozi wa Majlis Dawla.
Mhe.Naibu Spika akiwa katika mazungumzo na Naibu Spika wa Majlia Dawla ambalo ni Bunge la pili (upper house), Sheikh Yahya Mahfoudh Al Manthry wakati alipotembelea Bunge hilo nchini Oman akiwa katika ziara ya kibunge.
Baadhi ya watanzania waishio nchini Oman wakimsikiliza Naibu Spika Mhe.Job Ndugai (hayupo pichani) wakati alipokutana nao usiku wa Jumapili.Mhe Ndugai aliwahimiza watanzania hao kutosahau nyumbani Tanzania na kujitahidi kadri wawezavyo kutumia vizuri fursa zilizopo Oman kwa faida ya Tanzania.Aidha; Mhe.Naibu Spika aliwaeleza watanzania hao mambo mbalimbali yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kujibu masuala kadhaa waliyouliza.Naibu Spika amehitimisha ziara hiyo ya kibunge iliyokuwa na lengo la kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo baina ya mabunge ya Tanzania na Oman.
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.
unaweza kutupatia video ya maswali na majibu ya mkutano?
ReplyDeleteHahahaha!
ReplyDeleteMdau wa kwanza umeshuhudia Bunge letu likipanga kuratibu urushaji wa matukio ya Bunge ktk TV usiwe LIVE bali uwe unakuwa edited, labda Bunge la Oman wanaweza kutupatia video maswali hayo tukiwaomba !!!
Maswali na Majibu ya yaliyojiri huko Oman kwa Bunge letu utaambiwa ni Faragha (siri)...!!!
Jamani Masheikh wa nchi za wenzetu wanayaweza mambo angalieni wanaendesha hadi Mabunge!
ReplyDeleteIla sisi Tanzania mtihani wetu ni kuwa na Masheikh wa vurugu na Maandamano na ukorofi!
Oman kuna mabunge mawili la kwanza wabunge waliochaguliwa na wananchi la pili walioteuliwa na serikali na hili la pili ni wafanyakazi wakongwe kutoka all government institutions na huisadia serikali kujadili kila jambo linahusu maendeleo ya nchi na mwananchi. Yaani waliochaguliwa ni kama "Congress" na walioteuliwa ni kama "Senate" vyombo hivo hushirikiana kuboresha mwelekeo wa nyanja zote economy, ustawi wa jamii, elimu, kilimo na viwanda nk. Oman hatuna cha kuwafundisha watanzania ila tuna mifano mizuri mingi ya kuiga. Hoja kuwa hapa kwetu shekhe kazi yake msikitini kuelimisha jamii yanayohusu dini yao uchochezi haupo katika kamusi yetu kabisa watu wote ni sawa mbele ya sheria. Mweupe si bora kuliko mweusi wala mwekundu! Ukichunguza vizuri naibu spika wetu?(pichani) pia ni mweusi kwani hakuna weupe? Lakini hatuna ubaguzi wa rangi au dini asanteni.
ReplyDeletekuvaaa kanzau sio kitambulisho cha ushehe kama hujui jambo omba ufahamishwe hao mashekhe unawasema wanaendesha mabunge huko nchi za wezetu sio mashehe bali wamevaa kanzu kama vazi lao la taifa. na sheikh katika lugha ya kiarabu sio kiongozi wa kidini, ni kiongozi au mtawala.
ReplyDeleteIli kukumbushia tuu huyo aliyevaa joho ni naibu spika wa "senate" na hicho kivazi sio cha shekhe bali ni vazi rasmi la viongozi wanapokuwa katika safari za nje au nchini wakiwa wanapokea wageni ama mashekhe wanavaa kilemba cheupe na kanzu nyeupe ama akiwa katika shughuli rasmi kilemba cheupe na joho jeusi au kahawia. Shukran.
ReplyDelete