Jengo kuu la Ghorofa 5 ambalo lilikuwa halijamalizika ujenzi wake lililopo eneo la Sinza Mori karibu kabisa na Masjid Qubah,limeporomoka jioni hii na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa na wenzake wawili jirani na jengo hilo,ambapo mmoja alivyoona hatari hiyo alikimbia na kuwaacha wenzie wawili ambao walinasa ndani.

Kati ya walionasa mmoja amefanikiwa kutolewa huku akiwa ameumia vibaya na mwingine ndio huyo aliepoteza maisha.

Inasemekana chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo la Ghorofa ni hali yake ya kukaa kwa muda mrefu bila kumalizika kwa ujenzi waka ambapo inadaiwa kuwa lina umri wa zaidi ya miaka 10.

Habari kamili itafuata baadae kidogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Huu ni ujenzi wa chini ya kiwango, Hiyo sababu ya kukaa mda bila kumalizika haina msingi wowote! Tena lingemalizika ndio linge waua wengi tu!

    ReplyDelete

  2. Acha ushamba we anonymous wa kwanza nani kasema ujenzi wa chini ya kiwango?? gorofa imekaa miaka 10 bila kumalizika ujenzi wake lazima kusehemu za zege hua zainabaki wazi na kusubiria finishing ya kawaida ambayo isipo fanyika lazima jengo litaanguka

    ReplyDelete
  3. Nina ungana na Anonymous wa kwanza nina uzoefu na ujenzi, ni kweli hiyo yote inategemea na kiwango cha ujenzi... Kunamagorofa yaliyo jengwa kwa mda wa miaka 14 na haijaanguka, jee linge malizika na kuanguka ungeamini kuwa ni ujenzi mbovu.Jengo unapolijenga taratibu ndo linaongeza umri wake. Inawezekana kulikuwa na ufa kama unavyosema Anonymous wa pili, au hata matofali na cement alizozitumia mjenzi maana za siku hizi zinachakachuliwa sana. Ni heri kuzingatia matofali, cement, hata maji mtu anayotumia kujengea. Inasikitisha sana kwa maafa yaliojiri na tunamtangulizia maombi familia ya marehemu. Mwenye Jengo lazima akafanye uchunguzi wa kina kwaanzia kiwanja mpaka mjenzi aliyemtumia.

    ReplyDelete
  4. wewe umesomea wapi mambo ya ujenzi kiasi cha kumwita mwenzio mshamba na kusema ati limekaa miaka kumi bila kumalizika ndo maana likaanguka! Kiufupi hilo jengo limejengwa na vishoka! tunaanza kuiga ujenzi wa Wakenya huko nairobi kila wiki jengo linaanguka kwa ujenzi usiofuata viwango na masharti ya ujenzi!

    ReplyDelete
  5. Waachieni Engineers watumie ujuzi wao kutoa maelezo. Shida ya Sisi Wabongo tuna jibu la kila kitu, kila tukio!

    ReplyDelete
  6. Hayo ndo magorofa ya kichina.....tuachane kukumbatia vitu vya kichina jamani.

    ReplyDelete
  7. Anon wa pili (Feb 17, 10:59:00 pm 2013) ndo mshamba!! Kama base na nguzo za kiwango zilikuwepo bila hata kumalizika bado lingetakiwa kuwa imara. Finishing haina mchango mkubwa ktk uimara. VYOVYOTE VILE LILIKUWA CHINI YA KIWANGO!!! AFADHALI LIMEDONDOKA KABLA YA HIYO FINISHING AMBAYO INGEZIBA UBOVU TU NA KULETA MAAFA MAKUBWA ZAIDI YA YALIYOTOKEA!!

    ReplyDelete
  8. Naungana na Mdau wa Kwanza juu,

    Sababu ni Ujenzi chini ya Kiwango na bila kufuata mashariti ya Ujenzi.

    Kigezo sio kukaa muda mrefu likiwa ujenzi umesimama.

    Mbona katika maeneo ya Kihistoria kama Bagamoyo na Kilwa pana majengo yamepita zaidi ya umri wa Karne, lakini hayaanguki?

    ReplyDelete
  9. Kitendo kile kile unakuta cement mfuko mmoja kwa kalai nyingi za mchanga bila kujua adhari yake baadae ndio kama hivyo mwenye nyumba alijenga akijua yeye atapata faida zaidi sasa hapo ndio kama ilivyotokea sasa,ajifunze.

    ReplyDelete
  10. Mmiliki amekatikiwa na Mshiko atamaliza vipi ujenzi?

    ReplyDelete
  11. Zaidi ya Viwango vya Ubora havikuzingatiwa kwa Ujenzi chini ya Kiwango,

    Tatizo kubwa linalotukabili nchini Tanzania hatuna utamaduni wa Competitive Bidding hasa ktk Sekta Binafsi.

    Sio ajabu ukakuta Mkandarasi amepatika bila vigezo vya kiushindani na huenda ana majina moja ya haya:

    1.Kwetu Kumoja Co.Ltd.
    2.Tule sote Builders & Co.
    3.Dunduliza Contractors Ltd.
    4.Usinitupe nduguyangu Co.Ltd.
    5.Tujuane Builders Ltd.

    ...Mnaona ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...