JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Christopher Fuime alisema pia walikamata vifaa mbalimbali ambavyo walikuwa wakitumia kwa ajili ya kufanyia uhalifu huo.
Vifaa walivyokamatwa navyo
Vifaa vilivyokamatwa navyo ni kadi za bandia 194 za kuchukulia fedha katika ATM za Benki ya NMB, ambapo kati yake kadi 95 zilikuwa na namba 0225152975 zinazotumia namba ya akaunti ya 2258103695 zenye jina na picha ya mtu anayedaiwa kuwa ni mtumiaji mwenye jina la Molely L. P. Kadi nyingine 99 zilikuwa na namba 0506056317 za akaunti namba 5068000322 zikitumia jina moja la Mnuo Z. E na picha moja.
Pia walikutwa na kadi ya Benki ya Amerikani yenye namba 549012345678 zilizokuwa zikitumia jina la Richard Croswell.
Spray ya kupulizia Camera za usalama kwenye ATM
Picha na Gsengo Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wizi wa Digitali:

    Hii changamoto inabidi ikabiliwe ili tuwe na mazingira salama ktk fedha na Mabenki.

    NI WAZI YA KUWA KASI YA WIZI WA KISASA IPO JUU KULIKO TEKINOLOJIA INAYOTUMIWA NA VYOMBO VYA KIFEDHA NCHINI TANZANIA.

    Hakuna sababu kuendelea kutumia CCTV cables wakati Kasi ya Maendeleo ya Tekinolojia ipo juu sasa, inahitajika kutumia ya Sattelites kama Google+ na zinginezo ambazo hazihitaji hata kamera za kufunga ukutani!

    ReplyDelete
  2. Kiwango chao cha Usanii kimekomaa sana,

    Kufanya wizi hadi kwenye mizunguko ya nje ya Kifedha kama Mastercard na Visacard sio kitu kidogo.

    Pana uwezekano pia mkubwa ya kuwa wameshirikiana na watu nyeti ndani ya NMB sio bure!

    Hebu angalieni Mabenki ya Marekani yanapakuliwa fedha zao kwa Kadi zilizopo huku, ni padogo hapo?

    ReplyDelete
  3. tungependa kuwaona hao wezi kwa sura zao..umma uweze kuwatambua majangili yanaotaka kujipatia pesa kwa njia za shortcuts..

    halafu tunawaona kwenye mabaa wanatumia tu pesa ovyo ovyo...

    wangekua China hao ni kunyongwa tu basi.

    ila kwa nchi yetu utasikia hadi wafanye uchungzui tena..halafu kesi itaendeshwa muda usiozidi miaka minne..halafu badae utasikia wako tena mtaani..JAMANI TANZANIA!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...