Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akikata
utepe wakati wa uzinduzi wa hoteli mpya yenye hadhi ya nyota 4 ya palace
jijini Arusha jana.Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bw. Nehemia Mchechu na
kulia mmiliki wa hoteli hiyo Dr.Hans Macha.
waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
akiangalia jiwe la msingi baada ya uzinduzi wa hotel yenye hadhi ya
nyota 4 Palace hoteli iliyopo katikati ya jiji la Arusha.
WAZIRI
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka akikata
keki yenye taswira ya jengo la hotel ya palace pamoja na mke wa
mkurugenzi mkuu wa Palace hotel Bibi Vaileth ,Macha wakati wa uzindizi
rasmi wa hoteli hiyo.
WAZIRI
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka,naibu
waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu,Waheshimiwa Wabunge wa
Majimbo ya Arusha na Arumeru Mashariki,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Nyumba na Mkutugenzi Mkuu wa Hoteli hiyo waliongozana kuingia
ndani ya jengo la hoteli hiyo.
Watu mbalimbali wakati wa kufungua hoteli wakishuhudia.
WAJASIRIAMALI
nchini, wametakiwa kujitokeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii
nchini, ili kukabiliana na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika
hoteli za kitalii ambao unalikabili Taifa.
Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo
jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo
imejengwa kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC).
Lazaro
alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na
mapato,”mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na nchi ya
Rwanda na udogo wake ilipata wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni
upungufu wa vyumba vya kulala wageni”alisema.
Alisema
mkakati huo utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi
kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa kulala wageni ambapo kwa sasa ina
vitanda 2,800 tu nyuma ya mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na
kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda 900 licha ya ukubwa wake.
“Tunaomba
shirika la nyumba lijitanue hadi maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa
za kitalii…na sisi wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje
kujitokeza kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya hifadhi zetu
panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi wenye urasimu
wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema ujenzi wa hoteli hiyo
yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu kiasi cha sh 16 bilioni ambapo NHC
imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku kiasi kingine kikitolewa na Palace
Hoteli.
Alisema
mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa
makubwa, kutokana na uwazi katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza
mapato kwa pande zote NHC na Mbia.
“binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa
uwazi katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi
mingine aje tushirikiane”alisema Mchechu.
Naye
Dk Ha Macha alisema mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120
na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na
utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa.
“hoteli
hii tunatumia malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni
njia ya kuongeza ajira na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali
ikiwepo na utunzwaji wa mazingira”alisema Macha.
Akifungua
mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza
mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia
ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali.
Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani
katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka
kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151 milioni.
“natoa
agizo rasmi kwa wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama
hawajatekeleza hadi sasa basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa
shirika la Taifa”alisema Profesa Tibaijuka.
Hii hoteli ni nyota 5 au 4.the title and the story contradicts each other
ReplyDeleteWewe hujui kuwa hiyo ni dili ya muuza ngozi Daktari Hans Macha na Nyarandu? Inabidi waukuze hiyo hoteli ili ionekana kuwa ni ya juu.
ReplyDeleteWatakao lala hapo ni viongoziwa serikali na wala sio watalii, wewe utaona,
Pesa ya EPA hiyooooo !!!