Jamaa hawa ambao majina yao hayakuweza Patikana mara moja,walinaswa na Kamera ya Globu ya Jamii maeneo ya Kimanzichana Wilayani Mkuranga,Mkoani Pwani wakijaza mafuta aina ya Petrol kwenye vikopo vya maji na soda tayari kwa kuwauzia watu wanaotumia zaidi usafiri wa PikiPiki maarufu kama Boda Boda,kutoka kwenye Madumu.Sheli za Mafuta za aina hii zimekuwa zikitumika sana hasa katika maeneo yaliyo mbali na vituo maalum vya kuuzua Mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kama utapita tena njia hiyo waambie wachukue tahadhari kwanihilo nibomu kubwa. Hapo walipo petroli inachemka. Uwii

    ReplyDelete
  2. Hii nchi haina miiko, everything goes. Utakuta askari nao wanahusika ktk biashara hiyo. Ngoja moto ulipuke hapo! Weeee....

    ReplyDelete
  3. hii ni hatari kwa maisha yao na wanaoishi au kupita sehemu hizo.

    Hebu fikira hapo anapita mtu na sigara ilhali ndoo hiyo ina petrol kibao moto wa aina yake unaweza zuka.

    Kama kawaida askari na serikali wanalifumbia macho hili, kwa sababu linafanyika mbali na nyumba zao wanazoishi.

    ReplyDelete
  4. Petroli zinazouzwa sehemu kama hizi zinafaa kuwekwa kwenye magari kama Land Rover 109, Peugeot 404, Ford Cortina na magari mengine ya kizamani ambayo hayako 'sensitive' sana kwa ubora wa mafuta. Kwa wenye magari ya kisasa nawashauri wanunue mafuta katika vituo vyenye hadhi.

    ReplyDelete
  5. Mdhara ni makubwa sana hasa ya Kiafya kwa kuwa PETROLEUM ina toa mvuke ambao una alergies za magonjwa mengi sana ya kupitia hewa ya kupumua na magonjwa ya athari za ngozi!

    Usione ajabu huyo mhudumu hapo baada ya muda fulani ataanza kuugua na hatimaye kifo!

    Si mmeona jinsi maisha yalivyo mafupi ?

    ReplyDelete
  6. Leseni ya biashara iko wapi?
    Usajili wa biashara uko wapi?
    TIN iko wapi?

    Ahhh Mjini tabu lakini wenzetu Porini wanapeta!!!

    ReplyDelete
  7. bongo banaa..likitokea zali hapo wataanza kuilaumu serikali au rais..wakati ni ujinga wao wenyewe!!bongo tambararez..

    ReplyDelete
  8. Civilization has no meaning from the grassroots to the green pastures!
    It is nasty!

    ReplyDelete
  9. Hiyo ni petrol iliyopimwa kwa ajili ya pikipiki (bodaboda) tu, ni mara chache sana mtu akaweka nusu lita kwenye gari....na bodaboda hawawezi kuendesha mwendo mrefu kuja mijini kuweka mafuta...it is a service that serves their purpose...though it's dangerous for their lives!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...