Mshambuliaji wa timu ya FC Libolo ya nchini Angola, Joao Martins, akiruka juu kupiga mpira wa kichwa na kuifungia timu yake bao la kuongoza mnamo dakika ya 24 ya mchezo katika kipindi cha kwanza,wakati wa mchezo wao wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya Timu ya Simba kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa mchezo Simba ilechezia kichapo cha Bao 1-0 toka kwa FC Libolo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Simba ina vipaji lakini kwa makocha hawa na maneno mengi ya kisiasa ya uongozi wa Rage wasahau kabisa na wapo ktk hatari hata nafasi ya tatu ligi kuu huenda wasiambulie!!Mdau ughaibuni !!!

    ReplyDelete
  2. Japo mie ni yanga damu lakini kwa hili, simanzi yaniingia.Haya ndio mchezo msikate tamaa watani na muwe kitu kimoja.

    ReplyDelete
  3. Simba vipi tena?Siyo kawaida yenu kutolewa mzunguko wa Kwanza kwenye Mashindano haya.Fanyeni mazoezi ya nguvu kwa ajili ya mchezo wa marudiano.NEVER SAY NEVER IN FOOTBALL

    Mdau David V

    ReplyDelete
  4. Simba mpira hawajui ni kelele tuu,msingi wa mpira ni kuwa na malengo dhabiti,sasa wao wabatumia siasa kama tupo shule na kuhonga honga tuu,waangalie azam mwaka huu kombe laligi ya voda ni lao kama yanga na hao simba hawatatumia mihongo yao,azam oyeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Huyo langoni ni kipa wetu wa Msimbazi au la , maana urefu wa mwamba wa goli unamfanya aonekane hana kimo cha kimataifa kudakia timu ya mpira wa miguu.
    Mdau
    Mtaa-wa-watani

    ReplyDelete
  6. Rage atoke tu

    ReplyDelete
  7. Tatizo kubwa ni uongozi usiokuwa na mbinu wala mipango ya kueleweka, wanafanya kazi kwa mazoea na historia i.e. business as usual. Wapenzi wa Simba lazima wakubali kungojea uongozi umalize muda wao na upatikane uongozi mpya ndipo mafanikio yatawezekana.

    ReplyDelete
  8. Vipaji vipo simba lkn siasa nyingi na kufanya kiwango kuwa duni. Poleni simba

    ReplyDelete
  9. LIBOL....

    Ehhh jamani hili jina nalo?

    Mjomba Michuzi wewe unajulikana kuwa na uwezo mkubwa wa Tafsida kama ulivyo tushukia 'Mashimo ya Mfalme Suleiman', nafikiri leo umeteleza kidogo!

    ReplyDelete
  10. Ama kweli uzalendo umeanguka sana nchini!

    TFF mpo wapo?

    Na Uongozi Simba mpo wapi?

    Hadi mnakubali kucheza na Timu yenye jina hilo?

    Ina maana kwa jina lao endapo mnafungwa mnakuwa mnafungwa mara mbili, yaani mnafungwa magoli halafu mnafungwa kutokana na jina lao!

    Kama ingekuwa ndio mimi Raisi wa Msimbazi ile tu Fax inaingia Ofisini kuwa tumepangiwa kucheza na timu yenye ''jina hilo'', mimi ningeweka mpira kwapani halafu ninge andika barua kujibu fax kwa kauli ya kukataa kucheza na Timu hiyo ama nipangiwe Timu nyingine!

    ReplyDelete
  11. Duhhh Watani poleni.

    Ama kweli kitu kimezama kama jina lenyewe lilivyo!

    ReplyDelete
  12. Wakulaumiwa ni Rage.

    Bora Simba kama Mdau wa 10 juu anavyosema tungeweka mpira kwapani!

    Kwa nini akubali Timu iingie Uwanjani wa watu wenye jina kama hili?

    ReplyDelete
  13. Yanga wenzenu wameshakoga!

    Je, na ninyi mtakubali kukipiga nao hata frendi mechi?

    Jamaa bado hawaja ondoka vipi mpo tayari?

    ReplyDelete
  14. Mdau wa 13 anony wa Mon Feb 18, 02:44:00 pm 2013

    ..hao jamaa kwa jina hilo acha waondoke zao, sisi YANGA ahhh hapana, hatutaki!

    ReplyDelete
  15. Hizi Timu zikija zingekuwa Majina yanapitishwa Basata kwa maadili kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...