Kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo wa leo.
 Kikosi cha Mtibwa Sugar.
 Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba akichuana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi.
Wachezaji wa akiba wa Simba wakiwa awaamini macho yao wakati jahazoi la timu hiyo likiwa linazama
Golikipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Shariff akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mtibwa imeshinda bao 1-0. 

 Waamuzi wa mchezo wa leo wakitoka uwanjani
Kocha wa Simba, Mzee Patrick Liewig akitoka uwanjani baada ya mchezo.
Kwa hisani ya Habari Mseto Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. mbona National pako patupu? Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. majina ya wachezaji picha za timu ya Simba na Mtibwa waliocheza ni muhimu ktk kukamilisha habari.

    ReplyDelete
  3. May be the players don't understand the coach, what are the performance indicators in his contracts. For sure he has failed to meet any and therefore Simba should let him go. These foreign coaches are a waste of our monies, I am sure Jamhuri K can do a better job. Simba should forget 2012/13.

    ReplyDelete
  4. KUMBE MUA NAO NI TUNDA?....

    ReplyDelete
  5. mi sielewi! yaani Tz imeshindwa kutoa mafunzo kwa mchezo wa soka hata ku'import' kocha! Wengi wao wanaletwa vimeo tu na ni uharibifu wa feza. mpak vyuo vina elimu ya michezo lakini sijui hivyo vitengo vinafanya nini!
    basi labda mtaala uundiwe tume mpaka vyuo vikuu!

    ReplyDelete
  6. WAANGOLA bado wangalipo nchini Tanzania?

    Ni wazi inaonekana pana upungufu ktk utendaji wa Idara ya Uhamiaji kama alivyolalamikiwa Tapeli wa Mtaa wa Samora wiki ya jana!

    Wale Wa-Angola walioleta Maafa ya (LIBOL....) nadhani bado wanaendelea kutesa nchini kama anavyotesa Afisa Uhamiaji Tapeli Mtaa wa Samora, licha ya kuwa Uhamiaji iliwapa Visa kuja kucheza mechi moja na kurudi kwao lakini tunaona wanaendelea na kuzamisha tena (LIBOL...) lao!

    Angalieni Matokeo haya ya Mpira:

    1.Tarehe 17/02/2013
    (LIBOLO F.C)-1 SIMBA S.C-0

    2.Tarehe 23/02/2013
    YANGA S.C(LIBOLO F.C)-1 AZZAM SC-0

    3.Tarehe 24/02/2013
    MTIBWA S.C(LIBOLO FC)-1 SIMBA S.C-0

    Hivyo basi kwa Matokeo ya Mechi hizi tatu hapo juu tuna wasiwasi hawa WA-ANGOLA WANGALIPO WAMO NCHINI TANZANIA HAWAJARUDI KWAO!

    ReplyDelete
  7. Duhh ama kweli Msimbazi imelaliwa vya kutosha!

    Mibol,,, miwili (2) yote hiyo?

    Libol,,,, la kwanza (Jumapili) tarehe 17 Februari, 2013
    SIMBA S.C-vs-LIBOLO F.C


    Libol,,, la pili (Jumapili) tarehe 24 Februari, 2013
    SIMBA S.C-vs-MTIBWA F.C

    ReplyDelete
  8. Lololooo jamani!

    toke Waangola waingie nchini mpira wa Tanzania umekuwa ukishuhudia mibol.... tu, mibol...tu, ikizama kwenye nyavu za Timu zetu kwa kwenda mbele!

    Au tena ndio uchuro huo?

    ReplyDelete
  9. Kwa Jezi walizovaa Mtibwa?

    Hapa ni kuwa Simba imecheza na Yanga !

    MATOKEO:

    MTIBWA F.C(YANGA)-1
    SIMBA S.C-0

    Hivyo kwa jicho la tatu Simba imefungwa na Yanga!!!

    ReplyDelete
  10. Enheee!!!

    Mtani wangu Simba SC na hilo jana lilikuwa ni libolo la ngapi sasa?

    ReplyDelete
  11. hapana hapana hapana!

    sasa basi!

    kwakweli simba mtakuwa kila mechi mnapokea mibolo hiyo mpaka lini???

    !!!

    ReplyDelete
  12. Simba sc mmeshapokea libolo kutoka LIBOLO FC, halafu tena jana bila aibu tena kwa mara nyingine mnapokea tena libolo lingine kutoka MTIBWA FC!

    Sasa msubiri libolo lingine kutoka YANGA SC!!!

    ReplyDelete
  13. Kwiyo!, kwiyo! kwiyo,!(kiumbe/MNYAMA analia huku akiwa amebanwa hana uwezo wa kuchomoka akiwa amesha elekezwa Kibla)

    Kwachu!,kwachu!,kwachu!,(kisu kinanolewa kwenye jiwe kubwa)

    ....kwiyooooooooooooooooooo, orrrrrrgghhhhhhh ! (mnyama analia kwa uchungu huku kisu kimesha zama kwenye koromeo na mnyama anakata roho)

    Hatimaye mnyama ala KISU mchana kweupeeeeeeee!

    (MTIBWA F.C wanachukua kitoweo chao wanaweka kwenye kapu, huku mchinjaji akipewa shingo)

    Pyeeeee, pyeeeee , pyeeeeeeeeeeee!

    (FILIMBI YA MWISHO INAPULIZWA)

    WATU WANANYANYUKA KWENYE VITI VYA MAJUKWA UWANJANI WANA KUNG'UTA SURUALI ZAO WANARUDI MAJUMBANI KWAO!!!

    ReplyDelete
  14. Bora mngefungwa na LIPULI FC kuliko kufungwa na LIBOLO FC!

    Aiseee kuchapwa nao kunauma sana!

    Je Simba zile 5-0 na 'LIBOLO' mlilopata mara mbili (2) mwezi huu Februari-2013 NINI KINAUMA?

    ReplyDelete
  15. haya ndio matokeo ya maandalizi ya fasheni.ziara ya oman haikuwa kwenye programme ya simba ililazimishwa ili kushindana na yanga walioeka kambi uturuku.wenzao ziara hiyo ilikuwa kwenye programme ndiyo maana haikuathiriwa na kombe la mapinduzi wala kambi ya taifa stars,simba walikurupuka na matokeo yake wakaweka kambi ya wiki moja tu

    ReplyDelete
  16. Simba msikate tamaa kufungwa ndio mchezo, na haina maana ndio kushindwa. Wanafungwa Barcelona (Barcelona 0- Real Madrid 2, wanafungwa Man City (Chelsea 1 Southampton 3)lakini hawakati tamaa kuwania ubingwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...