Wachezaji wa simba, wakimpongeza kiungo wao Mwinyi Kazimoto, baada ya kuifungia timu yake bao, wakati wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha leo  jioni. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 1-1.

TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo jioni imevutwa shati na JKT Oljoro baada ya kufungana bao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Voidacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kwa timu ya Simba leo imetimiza sare ya pili tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare kama hiyo na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamm na kuifanya 
 Simba kutimiza jumla ya  pointi 28, baada ya kucheza mechi 16, huku watani wao Yanga wakiongoza kwa kuwa na pointi 33 na mchezo mmoja mkononi, wakati Azam FC ya pili wakiwa na pointi 30 na mchezo mmoja mkononi.
Bao la JKT Oljoro, lilifungwa na Paul Nonga, katika dakika ya tisa tu tangu kuanza kipindi cha pili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. I think my club should forget about the current League, they are basically gone for the year. A draw with a tea zat does not employ a multi million dollar coach and players - I just don't get it.

    Labada tuangalie mwakani.

    Simba supporter

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...