TAARIFA KWA UMMA
Tunasikitika kuwataarifu kwamba mnamo tarehe 3/02/2013 saa 12:00 asubuhi kulitokea ajali ya moto katika chumba cha mifumo ya mawasiliano kilichopo sehemu ya juu kabisa Jengo la PPF Tower lililoko makutano ya mtaa wa Ohio na Garden Avenue.
Moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa vikosi mbalimbali vya zima moto.
Zoezi hilo la uzimaji wa moto lilitumia kiasi kikubwa cha maji ambayo yalisambaa kwenye maeneo ya ngazi,mifumo ya umeme na mawasiliano.
Wataalamu wanaoshughulikia mifumo ya umeme wamefanya ukaguzi na kushauri kusitishwa kwa matumizi ya umeme katika jengo hilo mpaka watakapokamilisha zoezi la ukaushwaji wa maji hayo.
Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mapema iwezekanavyo.
Moto huo haukuathiri sehemu nyingine za jengo hilo zikiwemo ofisi za wapangaji. Tunaomba wapangaji,wadau na watumiaji wengine wote wa jengo hilo wawe wavumilivu wakati zoezi la ukaushaji wa maji hayo inaendelea na kisha umeme kurejeshwa ili waweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF

Jamani Mnatakiwa kujenga tabia ya KUKINGA kwa kukagua majengo yenu kwa utaratimu fulani zaidi ya hapo ni upuuzi mtupu. Pia ni wajibu wa mkurugenzi kujumuisha katika taarifa zake ni NINI ATAKIFANYA KUZUIA/AU KUPUNGUZA NAFASI KWA HALI KAMA HII KUTOKEA. Bila hivyo tnaendelea kuwa watoa taarifa baada ya matukio hasi kama haya.
ReplyDeleteBora wafanye mazoezi ya kupanda ngazi maana wamezidi vitambi.
ReplyDeletehuu ndio uungwana tunaoutaka. kukiri na kuomba radhi basi watu wenye utu watakuelewa tu.poleni PPF Tower,haya yapo lakini nashauri muwe mnakagua mifumo yenu mara kwa mara ili kuepuka yanayoepukika.
ReplyDelete