Kampuni yetu ya BEYOND EVENT ORGANISERS  inatarajia kuanza kuaanda matukio nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar-Es-Salaam. Kwa kuanzia tutaanza na tafrija ya chakula cha usiku chenye hadhi ya mahaba kwa wapendanao (ROMANTIC DINNER).
Naomba upitie link hii  http://www.surveymonkey.com/s/GSF9NTG ili uweze kutusaidia kuchangia maoni yako.
Madhumuni ya zoezi hili ni kujaribu kupata maoni yako ili tuweze kuboresha shughuli yetu na kuhakikisha kuwa tunakidhi matakwa ya wateja wetu.
Swali la tisa (9) linakupa fursa wewe ya kutueleza kwa kina yale unayofikiria ni muhimu katika kufanikisha shughuli hiyo. Kumbuka kuandika jina lako, nambari yako ya simu na anuani yako ya barua pepe (e-mail).
Kwa kufanya hivyo utapewa punguzo la Tshs 10,000/= wakati wa kununua tiketi yako pindi muda utakapowadia.
Nitashukuru kama utatusambazia ujumbe huu kwa marafiki zako, ndugu na hata wafanyakazi wenzio ili siku itakapowadia tufurahie kwa pamoja.
Regards,
MfundaYasini M.I.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. tukusaidie kufanikisha biashara yako halau utatoa elfu kumi tu kwenye kiingilio? je kiingilio cha couple au mmoja?

    bora ungesema nusu kwa atakaekushauri vizuri

    wengi mnaingia biashara bila kujipanga na kutegemes sie wengine halafu eti elfu kumi, duh.

    ReplyDelete
  2. Umeona eeeh,afanye akosee then ajifunze kutokana na makosa

    ReplyDelete
  3. PENZI KITOVU CHA UZEMBE!

    Watanzania tuelekeze jitihada zetu kwenye kazi na kujadili changamoto zinazotukabili badala ya kuelemea kwenye agenda za kuchangia uboreshaji Mapenzi, then so WHAT?

    Mapenzi kila kiumbe anayajua kwa njia zake,kwa wakati wake na upande wake hata njiwa ana mpenzi wake kwenye tundu!

    ReplyDelete
  4. You have not been told to invest your money, it's all about opinions. No wonder some of us don't progress kwa sababu ya wivu. Bravo bro, big up. Unafanya according to customers satisfaction!

    ReplyDelete
  5. Excellent idea brother. This is truly a modern way of introducing a new product into the market. Nimeisha kamilisha survey yangu. Nasubiri tu punguzo.

    ReplyDelete
  6. Hii kitu itakuwa lini? wacha tunaojua mapenzi tujimwage. Achana na hao wasio na kitu, kelele nyingiiii. Well done Bro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...