Balozi Ramadhani Mwinyi,Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kamati Maalum inayohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani C-34. Wakati wa mkutano huo Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa (DPKO), Bw. Herve Ladsous aliwataarifu washiriki wa mkutano huo, kwamba Idara hiyo ilikuwa ikijielekeza katika matumizi ya teknolojia za kisasa ( Unmanned Aerial System ) maarufu kama Drones katika operesheni za kulinda amani na kwamba teknolojia hiyo itafanyiwa majaribio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC)
Na Mwandishi Maalum
Wakati Idara ya Operesheni ya Ulinzi wa Amani ya Umoja
wa Mataifa (DPKO) ikijielekeza katika matumizi ya teknolojiza za kisasa katika
shughuli za ulinzi wa amani, zikiwamo
ndege zisizokuwa na rubani (Unmanned
Aerial Systems ) maarufu kama Drones. Baadhi ya mataifa hasa yale
yanayoendelea yanataka kuwapo kwa majadiliano zaidi kuhusu
matumizi ya zana hizo.
Taarifa ya matumizi ya teknolojia za kisasa katika
ulinzi wa amani, imetolewa na Mkuu wa
DPKO , Bw Herve Ladsous, wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa Kamati Maalumu
inayohusika na masuala ya operesheni za
kulinda amani maarufu kama C-34. Kamati
hiyo maalumu ipo chini ya Kamati ya Nne
ya Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika taarifa yake, Bw Ladsous ameeleza kwamba uamuzi
wa kutumia teknolojia za kisasa zikiwamo
unmanned aerial systems
(UAS) unalenga katika kuboresha utendaji
kazi wa misheni za kulinda amani, kukusanya taarifa na kutoa tahadhari za awali
na kubwa zaidi kuokoa maisha ya walinzi
wa amani dhidi ya hujuma mbalimbali.
Katika mwaka uliopitia (2012) walinzi wa amani 111
wakiwamo watanzania sita wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti kwa kushambuliwa wakati wakitekeleza majukumu yao ya kuwalinda
wananchi katika nchi zenye migogoro.
Akieleza zaidi kuhusu
mpango huo, Bw. Ladsous amesema,
zana hizo zitaanza kwa majaribio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
kupitia misheni ya kutuliza amani
MONUSCO
“Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa pendekezo la
kutumika kwa majaribio teknolojia hii
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo. Tunafanya kazi kwa karibu na
Baraza Kuu la Usalama , nchi mwenyeji, na wadau wengine kuhakikisha kwamba
walinzi wetu wa amani wanapata fursa ya kutumia teknolojia ya kisasa” akasema
Mkuu wa DPKO
Na kuongeza kwamba matumizi ya teknolojia hizo ni muhimu si katika kuwalinda walinzi wa amani bali pia
kuzijengea uwezo na maarifa misheni hizo.
Mkuu huyo wa
DPKO akaeleza zaidi kwamba mchakato
umeanza wa kuomba ridhaa kwa nchi mwenyeji, kuzijulisha nchi jirani,
mawasiliano na nchi zinazotoa walinzi wa
amani (TCC) na kuwauliza wauzaji wa zana hizo wale ambao wataonyesha nia.
Baadhi ya mataifa
yaliyoendelea ingawa yanakili
kwamba bado kuna hali ya sintofahamu na hofu kuhusiana na suala hilo,yanaunga mkono matumizi hayo
katika kile wanachoamini kutasaidia sana kupunguza vifo vya walinzi wa amani.
Hata hivyo baadhi ya nchi zinazoendelea na ambazo
zinachangia walinzi wa amani maarufu kama TCC,
zinasisitiza kwamba uamuzi wa matumizi ya zana hizo za kisasa ni lazima
yajadiliwe miongoni mwao . Ikiwa ni
pamoja suala la sheria na sera za matumizi ya zana hizo, raslimali fedha na teknolojia inayoambatana
na zana hizo.
Mkutano huu wa Kamati Maalum ya operesheni za kulinda
amani licha ya kujadili suala zima la
shughuli za ulinzi wa amani, unajadili
pamoja na mambo mengine changamoto mbalimbali zinazowakabili walinzi wa amani
na mfumo mzima wa utekelezaji wa
operesheni hizo.
Baadhi yachangamoto zinazojadiliwa ni pamoja na mkanganyiko wa dhamana wanayobeba walinzi wa
amani , uhaba na ufinyu wa raslimali
fedha na vifaa, dhana ya ulinzi wa raia, ushirikishwaji katika utoaji wa maamuzi ,
ushiriki wa wanawake hususani Polisi
wanawake katika ulinzi wa amani na mafunzo kwa walinzi hao wakiwamo pia Polisi, Magereza na Raia
Suala la malipo
kwa walinzi wa amani ni jambo ambalo pia limeendelea kutiliwa mkazo katika
mkutano huu, na karibu wazungumuzaji wote
ikiwambo Tanzania ambayo
iliwakilishwa na Balozi Ramadhani Mwinyi, Naibu
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Matifa.
Wazungumzaji
wote wametaka
na kusisitiza kwamba ni matumaini
yao kuwa mapendekezo yaliyotolewa na Kundi la Washauri kuhusu malipo ya walinzi wa amani pamoja na vifaa
yatafanyiwa kazi ipasavyo wakati Kamati
ya Tano ya baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa itakapokutana mwezi March mwaka huu.
Madini. JUzi zimeibiwa almasi zenye thamani ya $50 million kule brussells mbona hwatumii teknolojia jii ya drones kuwatafuta wahalifu wao.
ReplyDeleteKwa Mpango wa UN wa Drones Mashariki ya Kongo, hapa ndipo Mchawi atakapo kamatwa.
ReplyDeleteLabda abadilishe staili ya Uwanga wake au aache kabisa Ushirikina!
DRONES Mashariki ya Congo?
ReplyDeleteOhooo wataumbuka watu hapo?
Lakini UN cha muhimu msitumie Drones kwa kuuwa kama kwenye suala la Magaidi isipokuwa mzitumie kwa Upelelezi wa nyendo za watuhumiwa wa harakati hizo, mchukue ushahidi na wawajibishwe wahusika.
Hapo ndio watu wanao heshimkika wataonekana usiku na makoti marefu meusi Msituni !
Hmna kitu,drones zipo na zinatumika siku nyingi tu Afghanistan,Pakistan,Iraq,Somalia na hata ISrael wanazitumia kule Gaza lakini hazijatatua tatizo.
ReplyDelete