Sherehe katika mji wa Kharkiv, Ukraine, hivi karibuni ambapo kituo hicho kimeanzsihwa kuimarisha uhusiano wa Elimu, Utamaduni na Maendeleo kwa ujumla kati ya Ukraine na Afrika.
Mhe. Balozi Jaka Mwambi aliweza kuzungumza na wataalamu wa mambo ya Elimu kuhusu kusaini mkataba wa Elimu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ukraine ambapo wamekubaliana kuhuisha mkataba huo katika vipingele kadhaa kwa upande wa Ukraine.
Mkataba huo utaruhusu Watanzania wengi kusoma vyuo vya Ukraine, wanafunzi wa Ukraine kusoma Tanzania pia, maprofessa kwenda kufundisha Tanzania, kubadilishana uzoefu wa tafiti (research) mbalimbali na hata kubadilishana mambo ya kiutamaduni.

 Wanazuoni wa kiTanzania waishio Ukraine katika picha na Balozi wa Tanzania nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi na Msaidizi wake - Mhe. Mbarouk N. Mbarouk.
 Mhe. Vil Bakirov - Rector wa Kharkiv National University named after V.N. Karazin, Mhe. Irina Gagarina - Director of Ukrainian State Centre of International Education of Ukraine, Balozi wa Angola nchini Urussi, Mhe. Jaka Mwambi - Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini  Urussi wakipongezana kwa uzinduzi wa kituo cha UKRAINIAN - AFRICAN EDUCATION CENTRE.
Wanazuoni kutoka Nigeria, Tanzania, Tunisia na Kenya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Geeeeeeeeeeeeeeeee, waswahili hata Ukraine - next place itakuwa Mars

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...