Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Muji wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezeko la Thamani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.
 Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hizi nyumba mbona hazina nondo au washaongea na wezi?
    mdau.
    india

    ReplyDelete
  2. Mdau India,

    Asante sana. Mimi pia kitu cha kwanza nilichokiona ni hayo madirisha ya vioo yasiyo na nondo wala nyavu za mbu na mlango wa mbele usio na grill halafu juu una kioo. Hii architectural siyo ya Kibongo kabisaaaaa. Magumashi matupu.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa India, hilo dirisha ni maarufu kwa jina la Almunium na kioo chake ni aina ya one way (kwa lugha zetu za mtaani)ambacho mtu akiwa nje haoni ndani ila wa ndani anakuona. Hivyo ni vigumu kusema hakuna nondo wakati kioo chenyewe hakikurusu kuona ndani.

    ReplyDelete
  4. kioo kutokuruhusu kuona ndani haina maana kuwa Wataalamu hawata nusa. jamaa wananusa kuliko majibwa ya polisi. Ukwei unabaki pale pale nondo ni muhimu sana kwa huku kwetu na kama mdau wa India alivyosema hawa jamaa labda wameshaongea na wezi na wamepewa uthibitisho kuwa hawapitia maeneo.

    Mdau Mbande

    ReplyDelete
  5. Million 94 kwa nyumba hao wafanyakazi wanaruhusiwa kukatwa kidogo kidogo au ni malipo cash hapo hapo. Bei ni kubwa sana kwa mshahara wa mlala hoi kama mimi!

    ReplyDelete
  6. yaani hizi nyumba zimekaa kama choo ndio nitoe milioni 94 kununa??? huu ni utani sasa.smh!

    ReplyDelete
  7. Hili ni jipu . Watanzania hatuna huruma hata chembe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...