Kundi la Nyumbu madume wakiwa wamejikusanya pamoja Serengeti wakiangalia watoto wao wanavyofurahia mandhari ya Serengeti.

=======  ====== ===

Watalii wafurika Serengeti kushuhudia tukio la Nyumbu kuzaliana

Zaidi ya Watalii 16,500 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni miongoni mwao wakiwemo Watanzania 5,800 wamefurika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio adimu linalohusisha Nyumbu wapatao elfu nane (8,000) kuzaliwa kila siku.

Mwezi Februari kila mwaka ndipo msafara wa Nyumbu hufika katika eneo la kusini mwa Serengeti kwa ajili ya kuzaliana. Miongoni mwa wageni waliofika Serengeti mwaka huu kushuhudia tukio hili muhimu ni pamoja na watafiti wa wanyamapori na wanazoolojia wanasayansi maarufu sana ulimwenguni.
 
Msimu wa Kuzaliana katika Serengeti ni tukio la kipekee ambapo ni Serengeti pekee duniani ambapo wanyama hawa huzaliana kwa pamoja katika mzunguko wao wa mwaka mzima.

Msimu huu wa kuzaliana utadumu kwa muda wiki sita ambapo hadi kukamilika kwake inatarajiwa kuwa ndama wapatao 500,000 watakuwa wamezaliwa katika eneo la Serengeti ambayo ni hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania.Kinchosisimua zaidi katika tukio hili ni pale ambapo nyumbu hawahitaji kulala chini kwa ajili ya kuzaa bali tukio hili huendelea huku Nyumbu akiwa anaendelea kutembea na kula malisho ya majani hifadhini.

Cha kipekee zaidi ni pale ndama aliyezaliwa mara tu akishazaliwa, humchukua kati ya dakika mbili hadi tatu kuanza kurukaruka na kumfuata mama yake kwa kasi kubwa.

Hata hivyo miongoni mwa ndama hawa wanaozaliwa kipindi hiki, wengi wao wapo hatarini kuliwa na wanyama wakali wanaowawinda kwa hamu kubwa kwa ajili ya kujipatia chakula. Wanyama hawa maarufu kwa kuwinda ndama hawa ni pamoja na fisi wanaofikia 7,500 pamoja na simba zaidi ya 3,000 ambao wote hukodolea macho tukio hili kwa nia ya kujipatia mlo wao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...