Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano.

 “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo” .

Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.

(MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia mpaka 5%.

Mdee alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema “Kinachojitekeza sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa vidogo hawavipati , na zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai”.

Mheshimiwa Halima Mdee alimalizia kwa kusema anadhani ni wakati sasa kama taifa lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa kuwepo bajeti inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na soko, na kusisitiza uwepo wa mitaala inayoeleweka tofauti na hivi sasa ambapo waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na kujiandalia wenyewe mitaala. Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa walimu bila upendeleo kwa kila shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina walimu wa kutosha na pia uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.

Mahojiano yote yanapatikana katika: http://www.hulkshare.com/81arza49bg5c

Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali.
Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango na Mbunge wa Kawe Halima Mdee baada ya kipindi.
Fina Mango akimuuliza Halima Mdee swali wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Makutano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ewe kama vile ulikuwa kichwani kwangu. Niliposikia Waziri Makuu kaunda tume kuchunguza kushuka kwa elimu nilijiuliza hivi kwa nini tu wasijiulize kwa nini hawapeleki watoto wao kwenye shule za kata? Hizo sababu za wao kuchukuwa uamuzi kutopeleka watoto wao shule za kata ndio hizo hizo za elimu mbaya kwa hiyo hili linajulikana

    ReplyDelete
  2. mheshimiwa mbunge mbona na hizo shule za Academia watoto nao wamefeli huko kama swala ni kwamba watoto wa wakubwa wanapelekwa shule za Academia basi zingekua zinaongoza kwa matokeo mazuri lakini badala yake nazo hazina matokeo mazuri hilo sio tatizo mheshimiwa jiulize kwa nini shule za seminary ndio zinazofaulisha mkaangalie wenzenu wanafanya kazi gani kufundisha watoto

    ReplyDelete
  3. DAWA NI MOJA TU, SERIKALI ITAHIFISHE SHULE ZOTE ZA WATU BINAFSI ISIPOKUWA ZILE ZA KIKRISTO NA KIISLAM ZIBAKIE MIKONONI MWA HIVYO VYOMBO VYA KIDINI MAANA KWAO ITAKUWA NI RAHISI KUCONTROL, NA ZILE ZINGINE ZA WATU BINAFSI ZICHUKULIWE NA SERIKALI ZIWE MALI YA SERIKALI NA NAAMINI KABISA HAKUTOKUWA NA MATABAKA KATI YA MTOTO WA MASIKINI AU TAJIRI WOTE LAO LITAKUWA MOJA. WALIMU WALIPWE MISHAHARA MIZURI NA WAWE WAAJIRIWA WA SERIKALI. SHULE BINAFSI ZIPIGWE MARUFUKU NA ZA KATA ZIONDOLEWE.

    ReplyDelete
  4. Huyu Naye kachemsha cha kuongea tatizo sio Serikali kusomesha Watoto Academy bwana MP gani huyu? Japo kuwa sipendi Serikali wanayofanya kwa hili kachemsha, Tatizo

    WAZAZI hawafatilii maendeleo ya Watoto mambo mengi ya Maisha ndio yanawaweka mbali na watoto wao.

    FILAMU na NYIMBO- Filamu ambazo hazina maadili na Nyimbo zenye mistari duni nazo ndio zinawapoteza Watoto muda wao mwingi wanaona Filamu na Nyimbo na kusikia Radio tu wanajikuta wanaiga watu sio wakuigwa

    Documentary za Elimu kwenye TV kidogo Mazungumzo ya Maendeleo Kwenye TV au Radio siku hizi sio Sana Wazazi au Marafiki watu Wazima wakikaa wanaongea pumba tu za pombe na Uzinifu unategemea Mtoto ataiga lipi?

    Mikanda ya X imejaaa Movie za Mapenzi Uchafu tu na Mabaaa ndio imewazunguka Wabunge kazi zao kutupiana Lawama sio kupokea Lawama waweke sawa si Chadema si CCM si Wengine Wote. MZ

    ReplyDelete
  5. MHESHMIWA HALIMA KASEMA ANAYEMTAKA AJINADI NA KUTUMA CV YAKE ATAIPITIA NA KUONA KAMA ANAFAAA, KAZI KWENU WADAU KAMA KWELI ANAMAANISHA .

    ReplyDelete
  6. Wewe anon unaezungumzia mambo ya kushuka elimu sababu ya video, filamu, nk ni mmoja wa wanaoharibu huu mjadala kwa kifikiria watoto walioko mjini tu ambao ni asilimia ndogo sana. asilimia kubwa ya watanzania na wanaofeli wako vijijini ambapo hawana uwezo wa kupata hizo filamu, nk. Leo nimesikia watu wanalaumu Facebook, sasa ni kiasi gani cha watoto wanakwenda kwenye facebook? Watoto wa mjini (kwenye teknolojia) wanafaulu zaidi kuliko wa vijijini.

    Na vile vile kama teknolojia inasababisha kufeli kwa watoto basi nchi zenye access kubwa ya teknolojia kuliko tanzania na watoto wao vile vile wangefeli! Wao kwenye hizo nchi wanafahamu hayo mambo ya X na wanasoma vile vile. Fikiria hizi hoja mbili kabla ya kuharibu mjadala

    ReplyDelete
  7. HUO NI MTAZAMO WAKE MBUNGE SO MSIMPINGE ANAO UHURU WA KUTOA MAONI YAKE TUKICHANGANYA MAONI YA WOTE NA KUYAFANYIA KAZI TUTAFIKA TUTAKAKO KUFIKA

    ReplyDelete
  8. Shule za "academy" au "academia"? Lakini nimemuelewa, enzi zetu zilikuwa zinaitwa "English-medium" Nakumbuka Waziri wa Elimu nyakati fulani (Mungai kama sikosei) pale wizarani kwetu Elimu alijaribu kufuta haya majina na yatumike yale yanayopaswa tuu, yaani, so and so Primary School, na so and so Secondary School. Ilikuwa sio rahisi........

    ReplyDelete
  9. yani watanzania saa zingine tuna mawazo mgando na mawazo ya kimaskini sana sasa hamtaki watoto wasisome shule nzuri kila mtu ana uhuru wa kuchagua anataka asome wapi ,wanaosoma shule za academia siyo watoto wa viongozi tu kuna watoto wa kila mtu,tuache mawazo ya kizamani na kurudishana nyuma kimaendeleo,cha msingi ni kuboresha shule za kata full stop

    ReplyDelete
  10. Ukweli utamaduni wa elimu haupo Tanzania, haujajengwa! Si wazazi wala watoto wanaothamini elimu. Wazazi wanabemebelezwa kuwapeleka wazazi watoto shule- nimejionea mwenyewe katika mikoa mingi kwamba watoto wanofaulu kuingia form 1 hawaendi shule.Wa Hili ni tatizo Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Mtwara, Lindi na kadhalika.
    Sasa huyu mtoto anefaulu alafu mzazi anajivuta kulipa ada, kununua uniform na mahitaji mengine anapewa ujumbe gani hapa si ni kwamba elimu si muhimu? Na mikoa mingine hii in neema ya mazao ya kilimo (Iringa, Mbeya Rukwa n.k) lakini wazazi wanasingizia uwezo wakati wilaya zingine za mikoa hii hazikosi zao moja au jingine kutoka shambani kila mwezi kwa mwaka mzima!
    Katika karne hii eti wazazi bado wanshawishika na ujinga wa ving'ombe viwili eti mtito wa kike aolewe na kukatisha masomo.
    Uhamasihaji wa umuhimu wa shule haupo na watu wangelalamika zaidi wangekuwa wanauona umuhimu wa elimu kuhusu matokeo haya.
    Leo hii nchini India na Uchina kwa mfano kuna maeneo wazazi wanaanza kuomba nafasi kwenye chekechea mara wanapothibitishiwa kliniki kwamba mama ana mimba! Tanzania mpaka mzazi atishiwe na DC au diwani au mtendaji kuchukuliwa hatua za kisheria ndipo ampeleke mtoto shule. Tanzania mzazi anashiriki kukatisha masomo ya mtoto.
    Hlaima Mdee is just being a politician and I suppose she must attack CCM at every opportunity kwa sababu nae siku moja nataka chama chake kishike hatamu. Lakini ukweli culture ya knowledge, learning na education haijajengeka Tanzania ngazi zote. That is the root of the problem

    ReplyDelete
  11. Naunga na Mdau wa 4 hapo juu anony wa Sun Feb 24, 04:39:00 pm 2013

    Matokeo Mabovu ya Mtihani Kidato cha nne yanachangiwa na mambo makubwa matatu:

    1.MTAALA MBOVU:, ambao Mhe. mabatia alishatoa angalizo lake lakini akapingwa vikali.

    Ni kuwa Elimu inaendana na Kiwango cha Maendeleo kilichofikiwa na jamii husika kulingana na kasi ya Maendeleo Kisayansi, Kijamii, Kiuchumi na Kitekinolojia.

    Huwezi kutoa Elimu kwa mazingira ya mwaka 1978 wakati lilipokuwepo Shirika la Elimu Kibaha na TES (Tanzania Elimu Supplies) wakati tukiwa mwaka 2012 kwenda 2013!

    2.MADAI YA WAALIMU:, wamesha wahi kupiga kelele kuhusu madai ya stahili zao nakuvutana mara kwa mara na Mamlaka, hivyo wanaweza kutumia Mtihani huu kama fimbo yao kujibu mapigo.

    3.WANAFUNZI WENYEWE:, kama Mdau wa 4 hapo juu anavyoeleza wengi wamezama ktk maisha ya kujiachia na kushindwa kumudu Masomo kwa kujihusisha sana na masuala ya Kijamii kama Facebook,Mapenzi,Sinema na Miziki hivyo kupelekea kushindwa kujituma ktk Masomo yao.

    ReplyDelete
  12. Mh Umejitahidi kujieleza, lakini sisadiki maneno yako kuwa chanzo kinaweza kuwa ni viongozi kuto wasomesha watoto wao ktk shule za kata, shule za kata hazina muda si mrefu, viongozi wengi sidhani kama wanawatoto wadogo wakusoma sekondari kwa sasa, wachache ninyie ambao wengine mnawatoto na wengine hamna, lakini ninyi nyinyi wenye watoto wadogo mnawalipia watoto wenu mamilioni ya shilingi kwa shule za chekechea, ninao ninao wa fahamu ambao ni wabunge wa Chama changu cha CHADEMA, hebu tuanzie sisi kufanya kujirekebisha nandipo tukinyooshee chapa tawala kidole. Wabunge wengi wa Chama changu cha CHADEMA mmekuwa ammnanishi mnayo yasema kwa matendo yenu, mmepinga magari ya kifahari lakini ninyi mnatembelea magari ya anasa. Wengi wenu ninyi ni waongo. Onesheni njia kwa matendo bana.

    ReplyDelete
  13. Mhe. Mdee tunshukuru sana lakini ingefaa uje na Ilani zote 2 za Vyama vyote ili utakakokuwa unakosoa ya CCM utueleze ni vipi Chama chako (Chadema) kingefanya ili kuweza kukwepa yaliyotokea.

    ReplyDelete
  14. Suala hapa si sababu ya shule za academy au shule binafsi ama shule za kata au za serikali. Suala ni walimu,vifaa vya kufundishia,malipo ya walimu na migomo ya walimu.
    WALIMU- Shule nyingi zilizopata matokeo mabovu ziko za serikali ziko za binafsi ni ukosefu wa walimu, walimu kwa maana ya idadi pia kwa maana walimu wa kufundisha somo stahili na walimu wenye vyeti.
    VIFAA VYA KUFUNDISHIA- Huwezi kupata matokeo mazuri kama shule yako haina vifaa vya kufundishia.
    MALIPO YA WALIMU- shule nyingi zenye kuwajali walimu kwa malipo stahili ndizo zilizofaulisha wakati zile shule zilizo na matokeo mabovu ni zile zisizowajali walimu hapa pia zipo hata za watu binafsi
    MGOMO WA WALIMU- Serikali isikwepe lawama kuwa migomo ya walimu imechangia kupata matokeo mabovu kwa shule za serikali.
    Kwa utafiti wangu nimegundua kwamba shule nyingi hazina walimu. Shule zenye utaratibu mzuri ndizo zenye walimu wengi na waliobobea. kazi ipi kwa wakaguzi wa elimu wawe wanafuatilia shule hadi shule zote TZ ziwe za binafsi na za serikali na kuainisha mahitaji ya shule ,Je yanakidhi kuitwa shule?????? zingine zinakuwa shule jina tuu shule isiyokidhi mahitaji ufutwe maana wengine huanzisha shule kufanya biashara ya kupokea karo na si kutoa elimu stahiki.
    JohnJohn

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...