Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mahojiano na Mtangazaji wa habari za michezo wa Televisheni ya Super Sport,Bi. Carol Tshabalala katika mjadala kuhusu Tanzania inavyo jitahidi kupamabana na ugonjwa wa Malaria,mjadala huo ulifanyika kwenye kituo cha mikutano cha Sandton kilichopo jijini Johannesburg Afrika kusini.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF),Leodiger Tenga wakati wa mjadala wa kuhusu kupambana na malararia.kulia ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) akisaini mpira ikiwa ni ishara ya kupambana na Malaria kwakupitia michezo.wengine pichani kutoka kushoto ni Mama Tunu Pinda,Meneja wa mpango wa kudhibiti malaria nchini,Dkt. Ally Mohamed,Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dkt. Seif Rashid,Mwana muziki marafu nchini Afrika kusini na Balozi wa kupambana na ugonjwa wa malari,Bibi Yvonne Chakachaka na mwisho ni Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB).
Mama Tunu Pinda akisaini juu ya mpira ikiwa ni ishara ya kutumia michezo kupambana na malaria huku Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisaidia kumshikia.katikati ni Balozi wa kupamabana na malaria na mwana muziki marufu nchini Afrika kusini,Bibi Yvonne Chakachaka.
Baadhi ya Wadau waliohusika kwenye hafla hiyo.Picha na Chris Mfinanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...