
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013.

Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.

Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013

Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.

Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
NASEMA HIVI: HILI TATIZO LA KUCHINJA SI LA KIDINI ILA LA KUNDI LA WATU FULANI KWA SABABU ZAO BINAFSI AMBAZO NI KUPANDIKIZA CHUKI KATIKA TAIFA HILI, MI NI ISLAM UMRI WANGU MIAKA 72 MZALIWA WA MWANZA, NIMEWAJUA WA-KRISTO TOKEA NAPATA FAHAMU,KAMA NDUGU, JIRANI SCHOOLMATES NK. NA TUKIISHI KIDUGU,TOKEA NIPATE FAHAMU, NDUGU ZETU HAWA SIKUZOTE WANAPOTAKA KULA HATA KUKU TU MAJUMBANI KWAO BASI WALIKUWA WAKIJA KWETU KUOMBA WACHINJIWE,NA KATIKA KUDUMISHA UPENDO BAADA YA KUKU HUYO KUPIKWA HULETA SHINGO YA KUKU ALIYEPIKWA KAMA AHSANTE KWA MCHINJAJI, NA HILO LIMEKUWA LIKIFANYANYIKA HATA KABLA MIMI SIJAZALIWA, NA KWA HESHIMA ZAIDI HATA BUCHA ZA NGURUWE ZILIKUWA ZIKIWEKA MBALI NA MAKAZIA YA WATU, NA ISITOSHE UKIRISTO UKO HAPA NCHINI KWA MIAKA ZAIDI YA MIAKA 200HATUKUSIKIA KUWA KWAO NI HARAMU KULA NYAMA ILIYOCHINJWA NA MUISLAM, LAKINI NI DHAHIR SHAHIR KUWA WAISLAM NI HARAMU KABISA KULA NYAMA ILIYOCHINJWA KINYUME NA TARATIBU ZA KIISLAM, SASA LEO 2013 HILI LIMEZUKIA WAPI GHAFLA HII? HAWA NDUGU ZETU LEO 2013 IMEKUWA KWA0 KULA NYAMA ILIYOCHINJWA NA MUISLAM NI KINYUME CHA IMANI YAO? JAMANI TUTAKAFARI! AU NASISI TUNATAMANI KIDOGO TUPATE KAMA YALE YA LIBYA, TUNISIA EGYPT, NK, TUJUE YAKIANZA HAYAISHI? TUWAONE WENZETU MPAKA LEO HAWANA RAHA. JAMANI VIONGOZI WA DINI MSITUPOTOSHE, NYINYI NDIO MNAPASWA KUWEKA AMANI, NA VIONGOZI WA SERIKALI JAMANI KUWENI WAKWELI. MSIWAOGOPE WALETA FUJO.
ReplyDeleteTazania eehe, nchi yangu naipenda; Kwa nini mnang'ang'ania suala la mjadala huu, wakati hatujaweza hata kukidhi viwango vya kimataifa vya uuzwaji wa nyama? Huku ulaya kwa sababu ya usimamizi mbovu haya wamekula nyama ya farasi, na nyie mnao ng'ang'ania mtuchinjie mnaagenda gani? Haya na kitimoto itakuwaje?
ReplyDeleteJamani wakati mnadiscuss mambo hayo na haya mengine muyaangalie. Kwa mtizamo wangu, ni bora tuendelee kama zamani kila mtu ajichinjee kama anavyojisikia. Tanzania oyee....
sasa walimalizavipi,au walikubaliana je?maana haya mambo tusiyachukulie poa ujue.
ReplyDeleteswali ni kwamba kila kutakapoibuka ugomvi/kutokuelewana juu ya nan mwenye haki ya kuchinja waziri mkuu utaenda?lets say Kondoa au masasi au tukuyu kote huko utakwenda kusuluhisha?
ReplyDeletewhat i can say, we need to clear this up national wise , na sio kukaa na watu wa kieneo kidogo na kuwapatanisha...kesho wakiibuka wengine je?
mdau hapo juu umenena.hili suala inabidi litafutiwe suluhisho la kitaifa badala ya suluhisho la mkoa.tusisubiri na kwingine yatokee
ReplyDeleteKwani ni lazima kununua nyama iliyochinjwa na mtu wa dini nyingine, na je nani alisema Islaam kazi yao ni kuchinja nyama? tusipoteze lengo. tunaomba tuheshimiane na kila mmoja amwone mwenzake kuwa ana haki ya kuishi hapa duniani. Dini gani inasema uue kwa upanga?
ReplyDeleteMbona nchi za kiarabu kama Dubai wanamabucha yameandikwa Halal na mengine yameandikwa not good for muslim, kwa nini basi tusiwe na utaratibu huu ileweke na haya naona ni mambo ambayo yangeingia kwenye katiba maana tupo serious na muungano lakini kuna madogo ambayo yanaweza kuleta machafuko
ReplyDeleteWADAU MNALIKOROGA, MTALINYWA HILO! PRO-SHETANI, UTENGANO, DHARAU SIO? MDAU WA KWANZA KAELEZA VYEMA, NA MWENYE MACH HAAMBIWI ONA.
ReplyDeletePersonally I see this as a business opportunity. I will try to get capital and start a line of Halal Butcheries. Tembea uone. Haya mabo ya kujifungia ndiyo tatizo lake. Hakijaharibika kitu hapo anzisheni Hala butcheries.
ReplyDeletewenzenu huku ulaya wako wayahudi ambao hawali nyama au kuku aliyechinjwa na mkristo hivyo pamoja na kuwa myahudi haupendi uislam anamtafuta mwislam achinje nyama au kuku au ananunua katika maduka ya halal meat. Marekani ukienda supermarket mafreezer ya nyama za nguruwe yanakuwa magharibi na nyamanyingine mashariki. Ukichanganya duka litapigwa vita mpaka litafilisika.
ReplyDeletehuku ketu koo zimechanganyika dini, na ili muishi kwa amani mnakubali suluhu. Ama chakula hakitalika.
Mimi ni Muislamu na nina fahamu zangu na elimu yangu timamu.
ReplyDeleteMimi nasema, nyama ni nyama. Hapa ulaya na hata uarabuni, waislamu na wakristo na wayahudi wanakula kila aina nyama McDonald's na katika mahoteli. Sijasikia hata siku moja Muislamu au Mkristo akilalamika kuwa chakula ni haramu kwa kuwa sio "halal". Tukiangalia sayansi, tutaona kuwa nyama ya halal na sio halal yote inaenda sehemu moja na kutoka sehemu moja. Kama kuna sababu za kutosha za kisayansi kuwa kula nyama halal ni bora katika afya yako, basi tusingekuwa na magonjwa kama ya kisukari n.k. katika nchi zetu.
Udini katika nchi masikini ni sumu ya maendeleo. Tunatakiwa tujenge nchi sio kuuwana kwa sababu za kidini. Kama unataka kula nguruwe kula, kama unataka kula halal kula. Mimi nimeshawahi kupita uarabuni (Oman) na katika hii hoteli, wakati wa Ramadhan, kulikuwa na nyama ya nguruwe katika buffet yao na hamna mtu alilalamika.
Kwa Muamko wa Udini kazi tunayo nchini!
ReplyDeleteMdau wa 11 juu.
ReplyDeleteSuala la kuhitaji kitu Halal ni suala la Kiimani.
Hivyo mahitaji ya mtu yakimpelekea kiimani atumie Busara ili kuipata haki yake ya Kiimani ktk chakula.
Pia niliwahi kusikia ya kuwa ktk Madege ya nchi za Kiarabu ambako % kubwa ya wasafiri ni Waislamu huwa hata ktk Mwezi wa Ramadhan yanagawa vinywaji vyote hadi Pombe kwa abiria wake!
Hivyo, tuishi kwa kupeana nafasi na kuheshimiana, mla nguruwe ale nguruwe wake lakini aheshimu ya kuwa kuna Waislamu na Mayahudi ambao hawali nguruwe.
Pia wasiokula nguruwe waelewe ya kuwa jamii yetu imechanganyika na wenzetu ambao wanatumia tusichotumia sisi hivyo wapewe nao nafasi yao.
Pamoja kwa kuheshimiana tutaishi!
dah yaan wewe mdau wa Tue Feb 19, 06:51:00 am 2013 kama kweli waislamu wote wangekuwa na uelewa huu tungefika mbali nakupa like!
ReplyDeleteSisi binadamu tunasahau mambo haraka sana.
ReplyDeleteKatika vita vya nchi ya Yugoslavia, miaka ya 90, wananchi wao walilazimika kula nyama ya mbwa, paka na wanyama wote ili waishi. Kuna wakati binadamu pia anakula nyama ya binadamu mwenzake ili aweze kuishi.
Kama tunakua na njaa, basi utasahau hii halal na sio halal nyama, basi tu shida ya njaa sio kali. Mimi nakumbuka watu wanatumia sukari guru katika chai ya rangi wakati wa enzi za Mwalimu. Sasa tuna sukari ya kila aina.