Urban Pulse Creative inakuletea picha ya ziara ya Mh waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea makao makuu kampuni ya BG Group inayofanya kazi ya uchimbaji wa gesi na mafuta ili kuangalia ufanisi wake na jinsi gani itakavyoweza kutunufaisha sisi watanzania kama ikipewa fursa ya kuwekeza nchini kwetu.
BG group ni mojawapo ya kampuni kubwa duniani inayoongoza katika uchimbaji, utunzaji, usambazaji wa gesi asilia.Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 BG Group imeweza kujiimarisha zaidi kwa kujijengea uzoefu mkubwa na historia nzuri katika sekta hii nyeti ya nishati. Pamoja na kuwa makao yake makuu yakiwa mjini Reading nchini Uingereza vilevile kampuni hii ishafanya kazi katika nchi ishirini duniani ndani ya mabara matano tofauti ikiwa na wafanyakazi zaidi ya elfu sita kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Katika ziara hii Mh waziri Muhungo aliambatana na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, Mr Sosthenes Masau Bigambo Massola, Dr Athanas Simon Macheyeki (Geological Survey Tanzania), Mr Seleman Hatibu Chombo ( Idara ya Nishati na Madini Tanzania) na Mr Bikash Dawahoo mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza Tanzania

Makao makuu ya Kampuni ya BG
Mh Waziri Profesa Muhongo akipokea maelezo kutoka kwa injinia wa BG Group
Control room ya BG Group
Mh Waziri akifuatilia maelezo kutoka kwa msemaji wa kampuni ya BG ambapo ramani inaonesha live shughuli zainazoendelea katika visima vya gesi inayochimba nchini Tanzania
Mh Waziri akitembelea makao makuu ya BG Group
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris.
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris katika picha ya pamoja na ujumbe wake na wa kampuni hiyo
Sawa Prof. Muhongo kwa ziara ya Mjengoni Makao makuu ya BG Plc.
ReplyDeleteKwa hivi sasa licha ya mapungufu ni mengi masuala haya hapa ni ya muhimu kuharakisha:
1.Shughuli zinahitaji Mtaji mkubwa sana ili kuzisimamia wakati njia ya Mabenki na Mashirika ya Fedha yanatoa Mikopo ya Riba kubwa sana, huku umiliki wa rasilimali unahitajika zaidi ushikwe na Wananchi wa kawaida, NI MUHIMU KUFUNGUA UWEKEZAJI WA WATU WA KAIWADA KWENYE SOKO LA DHAMANA ZA MADENI (BOND MARKET) KITU AMBACHO JIRANI ZETU KENYA WAMEKUWA WANARUHUSU WATU WA KAWAIDA KUWEKEZA ILI KUKWEPA GHARAMA KUBWA ZA MAPESA YA MIKOPO YENYE RIBA ZA JUU.
2.Kuondoa Vipengele vinavyowabana watu wa kawaida kwenye ushiriki wa Masoko ya Hisa kama kiwango cha kununua Hisa kisizidi 60% ktk Masoko ya hisa.
3.Kuanzisha 'Dhamana Huru' yaani Sovereign Bond na kutoa ushirikishwaji wa Wananchi wa kawaida na pia kwenye umiliki wa rasilimali.
Mdau wa Urban Pulse-UK,
ReplyDelete...''Licha ya Kampuni ya BG kuwa na makao makuu READING Uingereza imeshafanya kazi ktk inchi zaidi ya 20 ndani ya Mabara ma 5''...
Sasa wewe ulitaka Makao Makuu yawe wapi?,,,kwa kuwa Kampuni ni ya UK ulitaka HQ iwe London?
Huu ndio ujinga wenu Wenezi, kama mlivyoitaka kuleta Mpango uwe Darisalama badala ya Mtwara!!!
Ni mimi Mkazi wa Mikindani-Mtwara.
Ashiii?
ReplyDeleteLicha ya Makao Makuu ya Bg kuwepo READING(MTWARA) wewe ulitaka yawepo LONDON(DAR ES SALAAM)???
Kwani Makao Makuu ya BG yakiwepo Mtwara itakuwa vipi?