Mhe. Mwansa Kapeya, Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji kutoka nchini
Zambia (wa pili kushoto) akiwa kwenye Picha ya pamoja na Prof. Makame
Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (wa tatu kushoto)
nje ya jengo la Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Dkt. Florens Turuka,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania na
Mhe. Elizabeth Phiri (wa kwanza kushoto), Naibu Balozi wa Zambia nchini
Tanzania.
Mhe. Mwansa Kapeya, Naibu Waziri wa Habari na Utangazaji nchini Zambia amefanya Ziara ya kujifunza nchini Tanzania kuhusu maandalizi na mafanikio ya kuwawezesha watanzania kuhama kutoka Teknolojia ya Utangazaji ya analojia na kutumia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali. Mhe. Kapeya alifanya mazungumzo na ujumbe wake Leo ofisini kwa Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Lengo la Ziara hiyo ya ujumbe huo kutoka Zambia ni kuona namna gani Tanzania ilijiandaa na kufanikisha kuzima mitambo ya analojia rasmi nchini tarehe 31 Desemba, 2012 kwa kuanzia na Mkoa wa Dar es Salaam ili nao waweze kujifunza na kuzima mitambo hiyo Kabla ya Desemba, 2013. Katika Ziara hiyo, Prof. Mbarawa alimueleza Mhe. Kapeya na ujumbe wake Kuwa ni vema Wizara yake iandae Mazingira mazuri ya kufanikisha uhamaji wa kutoka analojia kwenda dijitali kwa kuwashirikisha Wadau, sekta binafsi, wanasiasa, kutumia sera, Sheria na Kanuni na kuendesha Kampeni ya elimu kwa umma ili wananchi wafahamu umuhimu na manufaa ya kutumia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali. Ujumbe huo kutoka Zambia utakuwa nchini Tanzania kwa Ziara hiyo ya mafunzo Hadi tarehe 15 Februari, 2013. Na Prisca Ulomi, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...