Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Mzee mmoja mkazi wa eneo la Kitopeni mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar Bw. Ali Khamis Ali (65), ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja, ACP Ahmada Khamis, alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8.00 mchana huko kwenye eneo la Kitope mashambani.

Alisema Marehemu Mzee Ali, alikuwa amekwenda shambani kwake kukagua mazao yake ikiwemo minazi.

Amesema alipofika shambani hapo aliwaona vijana waliokuwa wakiangua nazi na wengine wakiwa chini ya mnazi wakiziandaa ili kuondokanazo kwa maana ya kuziiba.

Kamanda Ahmada amesema baada ya Marehemu kuwabaini wezi hao, inaonekana kuwa alianza kupandana nao lakini walimzidi nguvu na kumchona na kitu hicho chenye ncha kali ambacho kinaaminika kuwa ni kisu.

Amesema eneo la tukio walikuta rungu na ala la kisu kinachoaminika kumuulia marehemu. Amesema eneo la tukio hilo pia kulikuwa na damu nyingi na lilikuwa limevurugwa kutokana na mapambano.

Kamanda alisema baadhi ya wananchi wameitambua rungu hiyo kuwa ilikuwa ya marehemu aliyokuwa akiitumia kwa kulindia mazao yake ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiibwa na wezi.

Kamanda Ahmada amesema kuwa pamoja na marehemu huyo kuuawa lakini inaonekana pia mmoja wa wezi hao wa mazao naye amejeruhiwa katika mapambano hayo kwani kulionekana michirizi na matone ya damu ya mtu aliyeondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana. Amesema uchunguzi wa tukio hilo umeanza na amewataka wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona watu ama mtu mwenye majeraha ili akamatwe kwa kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda Ahmada alisema kuwa mauaji hayo ni ya kuwania mali na ametaka kutohusishwa na hisia za imani yoyote ama za kisiasa, kishirikina, wivu wa kimapenzi, kulipiza kisasi ama imani za kidini.

“Haya ni mauaji ya kawaida na hayana hisia zozote. Ni mauaji kama mauaji mengine yanayotokea katika maeneo mengine ya nchi yetu.” Alisema Kamanda Ahmada na kuwaonya wananchi kutoweka hisia tofauti na tukio lenyewe.

Amewaomba pia Waandishi wa Habari kutoweka maoni yao binafsi wanaporipoti taarifa za tukio hilo ili kuepuka kuwatia hofu wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Imamu wa msikiti wa kitope kauliwa , ety polisi wanasema ameuliwa na wizi wa nazi , nyie polisi munatupeleka wapi?

    Huyu ni imamu wa Msikiti kwa kuwa muislamu sio? Ingekuwa mkiristo yangekuwa maneo tele .

    Kisha unasema ety mauwaji haya hayana hisia zozote

    ReplyDelete
  2. Hahaaaa eti wezi wewe issamichuzi mjinga sana

    ReplyDelete
  3. Kwani imamu hawezi uliwa na wezi wa nazi?
    Tuache kuzipenda vurugu na mauaji.

    ReplyDelete
  4. mijitu mingine sijui ikoje? sasa mnalazimisha iwe kwammba kauliwa nanani na wa kristu au mbona hamtaki kuelewa?kila mtu sasa hivi akifa akiwa mwislam tuseme ameuwawa na wakristu.akiwa mkristu kauwawa na waislam.halafu iweje?sini ujinga huu kwanini msiache sheria ifwatwe watu wakamatwe.mtajua kila kitu.acheni kujiona kama dini fulani inaonewa wakati hili swala lipo kwa dini zote.tumieni akili.

    ReplyDelete
  5. anon wa sun Feb 24, 08:25:00 am 2013,

    nakubaliana nawe lakini hapo hapo ingelikuwa sawia kama kifo cha padre nacho kingeliripotiwa kuwa kuna sababu nyingi na sio za kidini.

    Padre kauliwa na vyombo vyote vya habari vinasema ni udini, shekhe ameuliwa vyombo vya habari kwanza haviseme kama huyu ni shekhe na pili hawasemi kama na mauaji haya ni ya udini.

    Hili ndio tatizo la vyombo vya habari vyetu havisemi ukweli kabisa. Vifo vyote viwili huenda vikawa ni vya kidini au ni wizi, pia huenda vikawa ni ugomvi baina ya marehemu na waliowafanyia mauaji. ukweli utajulikana watakapopatikana watuhumiwa, hivyo ndivyo vyombo vya habari vilitakiwa kuripoti na sio to make a conclusion kwa jambo wasililolijua ukweli wake.

    msema ukweli

    ReplyDelete
  6. shida ni kuwa kama una mazoea ya kufanyia wenzio mabaya hata usipofanya basi unahisiwa umefanya...haya yanayotoke na ni matokeo aya matendo yetu ya nyuma.Mbegu zillizopandwa za udini ndio zimemea sasa.

    ReplyDelete
  7. UKIWA NA TABIA YA WIZI HATA KAMA SIKU HIYO HUKUIBA WEWE UTAONEKANA TU KUWA WEWE NDIO UMEIBA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...