Pichani ni Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.SalimHemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
======= ====== ======
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaelezwa kuwa
aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chambani-Pemba, Salim Hemed Khamis,ambaye hapo jana
alianguka ghafla jijini Dar Es Salaam alipokuwa akihudhuria vikao vya kamati ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa hospitali ya Taifa
Muhimbili kwa matibabu, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali hiyo ya Taifa
ya Muhimbili,aidha chanzo cha habari hizi kimeongeza kuwa taratibu za
kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema
Peponi-Amin
inna lillah wa inna illayhi rajium, Muumba amweke katika kundi la waja wema
ReplyDeleteMungu amlaze pema Langu ni hili Yaani ni aibu kUBWA TANZANIA basi tunasihdwa hata kuwa na gari la kubebea wagonjwa katika offisi za bunge? au hata daktari mmoja maeneo muhimu hayo.
ReplyDeleteAaama kweli
natoa mkono wa pole kwa wafiwa na taifa kwa jumla,pia ningeomba kuwe na mpango maalum wa kuwapima wabunge wote afya zao uelewa wangu si wao tu majuzi nilifiwa na mjoba wangu amabe alikuwa ana bllod pressure lakini hamna aliyekuwa akijua pamoja na yeye mwenyewe tulijua baada ya kuanguka na baadae kufa.
ReplyDeletekwa tanzania ni jambo la kawaida ndio maana tuna ule msemo wetu wa kawaida "kafa ghafla" hamna hiyo ni uchunguzi wa kawaida wa afya ili tuweze kutumia kinga.
mungu amlaze mahala pema amin.
mdau.
dodoma.
Ameen @anonymous 1....
ReplyDelete