Spika
wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa
Chambani, Pemba, Mhe. Salim Hemed Khamis (CUF) - pichani -kilichotokea leo mchana katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili. Marehemu Khamis, alilazwa jana katika Hospitali
hiyo baada ya kuanguka ghafla akishiriki vikao vya kamati za Bunge
vinavyoendelea katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.
Marehemu
ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
alikimbizwa Hospitalini na kulazwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi
Muhimbili baada ya kubainika kuwa alikuwa amepata kiharusi kufutia shinikizo la
damu lililopelekea kuanguka kwake ghafla akiwa katika majukumu yake katika
Kamati za Bunge. Kutokana na Msiba huu, Shughuli zote za Kamati za Bunge
zimearishwa hadi jumanne tarehe 2 Aprili, 2013.
Marehemu
ataangwa kesho tarehe 29 Machi, 2013 saa mbili na Nusu Asubuhi katika Ukumbi wa
Karimjee, Dar es Salaam na kusafirishwa kwa ndege kwenda Pemba Saa Nne Asubuhi
ambapo Mazishi yatafanyika nyumbani kwake Chambani, Pemba Mchana. Mhe. Spika
anatoa Pole kwa Familia ya Marehemu, wananchi wa Chambani, Wajumbe wa Kamati ya
Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Wabunge wote na Watanzania wote kwa
ujumla.
Mungu
alilaze Roho ya Marehemu, Mahali Pema Peponi, Amina!
Imetolewa na
Idara ya Habari, Elimu Kwa Umma na Uhusiano wa
Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
28 Machi, 2013
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin. Kwa kwelini habari ya kisikitisha.
ReplyDeletePoleni wanafamilia. Poleni wananchi wa Pemba.
Mungu amlaze mahali Pema Peponi Amin
ReplyDeletekifo hakina ratiba michuzi!! rekebisha kichwa cha habari
ReplyDelete