MTU ANAESADIKIWA KUWA NDIE MUUAJI WA PADRI EVARIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI VISIWANI ZANZIBAR AMEKAMATWA ALASIRI HII MAENEO YA KARIAKOO, ZANZIBAR.

JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO,NA KWENDA NAYE KITUONI KWA AJILI YA MAHOJIANO ZAIDI.


PADRI MUSHI ALIUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MWEZI ULIOPITA WAKATI AKIWA KWENYE GARI LAKE KUELEKEA KANISANI KWENYE IBADA YA JUMAPILI. IFUATAYO NI SEHEMU YA TAARIFA YA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBA AFANDE MUSA A.MUSSA ALIYOITOA KWA WANAHABARI LEO,

Taswira ya kuchora ya mtuhumiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Amen mungu tenda

    ReplyDelete
  2. Nakubali anyongwe adharani tukimshudia nasio kumweka ndani miaka kibao anyongwe bac nasio mashine katani. Ndio tutakomesha hayd matatizo

    ReplyDelete
  3. Ili kuonyesha serikali iko makini ni vizuri mtu huyu ambaye naamini hayuko peke yake wapate adhabu kali na kesi yao iwekwe bayana ili ndugu zetu wakristo wapate imani.

    ReplyDelete
  4. Ni vizur mtu huyu pamoja n wote waliohusika wachukuliwe hatua ili kukomesha matukio ya aina hii

    ReplyDelete
  5. hii taswira kweli imesaidia kumkamata huyu mtu? mbona hii taswira inafanana na kila mwanamme wa makamo?

    ReplyDelete
  6. hiyo picha mbona imefanana na mimi kabisa na wala zanzibar sijawahi fika naishi shinyanga tangu nizaliwe.
    mdau.
    shinyanga.

    ReplyDelete
  7. Huyu mtu hadi muda huu bado tu ni mtuhumiwa hadi hapo atakapotiwa hatiani na mahakama baada ya kupatikana kwa ushahidi uliokosa mashaka (verification of evidence beyond reasonable doubt), cha ajabu ni kwamba tayari jamii imeshamtia hatiani mtu huyu tena eti kwa kufanana na picha tu!!!!
    Huko ulaya miongo kadhaa iliyopita kulikuwa na Waziri Mkuu aitwae Olof Palme (wa nchi ya Sweden) muuaji wake alitafutwa kwa njia kama hii ya mchoro, wengi walifananishwa lakini hadi leo zaidi ya miaka 25 hakuna aliyepelekwa mahakamani kwa kuwa tu ushahidi haukujitosheleza!! Ni lazima tuwe makini sana ili tuepuke kumuadhibu asiyehusika tena kwa dhana tu.

    ReplyDelete
  8. MH, HII PICHA HAPANA JAMANI KHA! NO ENOUGH DETAILS KWAKWELI., ITS TOO GENERAL BORA HATA INGEKUWA NI 3D.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2013

    Picha ni muhimu sana kupata pa kuanzia.watu wa muonekano huo wanaweza kuwa hata 100.Ila kwa kutumia taaluma ya watu wa intelligensia wanajua wanampataje.Tusiwe na wasiwasi wa mtu kutuhumiwa kwa makosa ambayo siyo.Wengine huwa wanakiri wenyewe wakishakamatwa.Tuwape muda vyombo vya dola wafanye kazi zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...