MKUTANO WA DHARULA WA WANACHAMA NA WADAU WA KLABU YA SIMBA YA JIJINI DAR LEO UMEAMUA KUUENGUA MADARAKANI UONGOZI WA JUU WA KLABU HIYO AMBAO UNAONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE NDUGU ISMAIL ADEN RAGE AMBAYE YUPO NCHINI INDIA KWA MATIBABU HIVI SASA.
MKUTANO HUO AMBAO UMEFANYIKA LEO HII JIJINI DAR UMEAMUA KUCHUKUA JUKUMU HILO LA KUWAONDOA MADARAKANI VIONGOZI HAO WA JUU BILA KUHUSISHWA MWENYEKITI WAO HUKU UKICHUKUA UAMUZI WA KUIKABIDHI TIMU HIYO MIKONONI MWA NDUGU HANS POPE NA MAMA RAHMA AL KHAROOS MPAKA HAPO UCHAGURI RASMI UTAKAPOFANYIKA.
TAARIFA KAMILI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...