Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Vick Bishumbo (wa pilikulia) akimkabidhi jezi mojawapo itakayotumika kama zawadi katika mashindano ya Gambo Cup, mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete MNEC, wengine katikapicha ni mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto) na meneja wa tawi wa benki ya NMB Korogwe Erasto Mwamalumbili,
 wameshika jezinyingine nyekundu.
  Ridhiwani Kikwete akiwa amepokea zawadi nyingine ya mpira.
 Mkuu wa Wilaya ya Korogowe Mrisho Gambo akizungumza  kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
 Ridhiwani Kikwete akiwa ameshika kombe atakalokabidhiwa bingwa wa michuano hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa
 Mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete akiongea.


Habari na picha na MashakaMhando,Korogwe
BENKI ya NMB imetoa vifaa vya michezo vitakavyotumika kama zawadi kwa washindi wa mashindano ya kugombea kombe la Gambo 'Gambo Cup' iliyofunguliwa wilayani hapa mwishoni mwa wiki, vifaa ambavyo vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 4.5.

Akikabidhi vifaaa hivyo kwenye ufunguzi wa mashindano hayo yaliyozinduliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bagamoyo, Ridhiwani Kikwete Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa benki hiyo, Vick Bishumbo alisema benkihiyoimetoa vifaa hivyo kama sehemu ya kusaidia jamii katikasekta ya michezo.

Alisema benki hiyo imekuwana utaratibu wa kusaidia jamiikatika sehemu kuu tatu ambazoni kusaidia katika huduma za elimu,afya na michezo ikiwani kutambua kwamba wao kama taasisi inayoshughulika na utunzani wa fedha za wananchi,wanalojukumu ya kuhakikisha inasaidiana na serikali katikakuhakikisha wanasaidia jamii katika sehemu hizo.

Meneja huyo wa kanda alitoa wito kwa jamii kutumia fursa ya mikopo inayotoa benki hiyo katika matawi yake 149 yaliyosambaa nchi nzima ili waweze kupambana na umasikini kwa kuinua kipato chao ikiwemo kukuza mitaji yao.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu zipatazo 79 za wilaya hiyo ya Korogwe,Mkuu wa wilaya hiyo Mrisho Mashaka Gambo, alitumia nafasi hiyo kuipongeza benki ya NMB kwa kuweza kusaidia sehemu za zawadi kwa timu hizo hatua ambayo inatakiwa kupongezwa na wapenda michezo wilayani humo ikiwemo taasisi nyingine kuiga mfano wake.

"NMB ni taasisi ya mfano ni moja ya taasisi ya kuigwa kwani imejitoa kusaidia jamii, sisi wana michezo tunajua ndiyo iliyokuwa chachu ya kuisaidia timu yetu ya Taifa, leo hii wamekubali kutusaidia wananchi wa Korogwe katika michezo yetu hii," alisema Gambo.

Mwenyekiti wa Chama Cha soka wilayani Korogwe (KDFA), Peter Juma alisema lengo la michuano hiyo itakayochezwa kwa vituo vinane vilivyopo wilayani humo itakayochezwa kwamtindo wa ligi, ni kuibua vipaji ikiwemo kuwatoa vijana katika masuala ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

Akizungumza katika ufunguzi huyo Ridhiwani Kikwete, aliwataka vijana watakaoshiriki mashindano hayo kutumia nafasi hiyo kuinua viwango vyao vya uchezaji ili mwisho wa siku waweze kucheza katika timu kubwa ambazo zitawasajili na kujipatia kipato kwa vile sasa michezo ni ajira.

"Michezo ni ajira,michezo hujenga mahusiano tudumishe nidhamu ili mwisho wa siku tuweze kukuza viwango vyetu ambavyo vitatusaidia siku za mbeleni, tunaweza kusajiliwa na timu kama Yanga na nyingine," alisema Ridhiwani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...